Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Majeshi Urusi yateka mitambo ya nyuklia Ukreini, mataifa yaonya
Kimataifa

Majeshi Urusi yateka mitambo ya nyuklia Ukreini, mataifa yaonya

Spread the love

 

UKREINI imesema majeshi ya Urusi yameshambulia na kuteka mtambo wa kuzalisha nishati ya nyuklia wa Zaporizhzhia ambao ni mkubwa zaidi barani Ulaya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Wasimamizi wanaendelea kufuatilia hali ya uzalishaji wa nishati,” zimesema mamlaka za mitaa katika mitandao ya kijamii na kunukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Imeripotiwa kuwa mapema leo moto mkubwa ulilipuka katika mitambo hiyo kufuatia mashambulizi ya makombora ya Urusi.

Kikosi cha kutoa huduma ya dharura kilifanikiwa kuuzima moto huo ambao uliwaka nje ya jengo lililopo eneo la mtambo.

Viongozi wa dunia wameishutumu Urusi kwa kujaribu kuhatarisha bara zima la Ulaya kwa kushambulia mitambo hiyo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema mashambulizi ya “kizembe” ya Urusi yanahatarisha usalama wa bara zima la Ulaya.

Naye Rais wa Marekani, Joe Biden ameitaka Moscow kusitisha shughuli za kijeshi karibu na eneo hilo wakati Waziri Mkuu wa Canada, Justine Trudeau amesema “mashambulizi ya kuogofya” kutoka Urusi “lazima yasitishwe mara moja”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!