SERIKALI ya Baraza la Jiji la Nairobi imetwaa majengo ya Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) kutokana na kutolipiwa kodi. BBC
Baraza hilo limeweka bango kubwa katika lango la majengo hayo kutangaza kwamba, kwa sasa majengo hayo yako chini ya usimamizi wa baraza hilo.
“Wapangaji wote wanafaa kulipa kodi kwa Baraza la Jiji hadi malimbikizi ya kodi yalipwe,” tangazo la baraza hilo limeeleza.
Baraza la Jiji linasema, linadai kodi ya jumla ya Dola za Marekani 20 milioni.
Hii si mara ya kwanza kwa baraza hilo kutwaa usimamizi wa majengo jijini Nairobi kutokana na kutolipiwa ambapo si jambo la kawaida kwa mashirika ya serikali kuandamwa.
Taarifa za ndani zinaeleza kwamba, shirika hilo la utangazaji limekuwa likikabiliwa na matatizo ya kifedha katika miaka ya karibuni.
More Stories
Kizza Besigye aachiliwa kwa dhamana Uganda
Mgombea urais aahidi kuuza korodani za fisi China
Uchaguzi Kenya: Raila na Ruto watofautiana kuhusu usajili wa wapiga kura