Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Majembe mapya Yanga yaanza mazoezi Morocco
Tangulizi

Majembe mapya Yanga yaanza mazoezi Morocco

Spread the love

 

KIKOSI cha klabu ya Yanga kimeanza rasmi mazoezi yake kujiandaa na msimu mpya wa mashindano jijini Marrakesh nchini Morocco, mara baada ya kuwasili siku ya jana, huku wakiwa na wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Yanga italazimika kutimia siku 10, nchini humo ili kujiweka sawa kabla ya kurejea nchini Agosti 27, kwa ajili ya tamasha la siku ya Mwananchi litakalofanyika Agosti 29, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga kilianza safari ya kwenda Morocco Agosti 15, 2021 kupitia Dubai na kisha kuwasili nchini humo Agosti 16, mwaka huu na siku ya leo walianza mazoezi rasmi.

Mazoezi hayo ya Yanga yalisimamiwa chini ya kocha wao mkuu Mohamed Nassridine Nabi, ambaye alitangulia nchini Morocco akitokea mapumzikoni kwao nchini Tunisia mara baada ya msimu wa Ligi kukamilika.

Yanga imenza kujifua ikijuafika kuwa itacheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inaytarajia kuanza Septemba 12, mwaka huu kwa michezo ya awali mara baada ya kupangiwa klabu ya Rivers United kutoka nchini Nigeria.

Katika kuhakikisha wanafanya vizuri, kwenye michezo hiyo uongozi wa klabu ya Yanga ulimau kuingia sokoni na kufanya usajili wa nguvu kwa kusajili jumla ya wachezaji 11, watakaongeza nguvu katika idara zote na kupelekea timu hiyo kufanya maandalizi mazito nchini Morocco.

Katika kuanza maandalizi hayo nchini Morocco baadhi ya wachezaji wapya tayari wameshaanza chini ya kocha Nabi huku wengine wakitarajia kujiunga na kambi hiyo hivi karibuni.

Wachezaji wapya ambao mpaka sasa tayari wameshaanza mazoezi ni Heritier Makambo, Fiston Mayele, Jesus Moloko, Djuma Shabani hao wote kutoka nchini Congo.

Wengine ni Djigui Diarra, Dikson Ambundo, Yusuph Athuman, Erick Johara na David Brayson huku Kharid Haucho na Yannick Bangala wakitarajia kujiunga na wenzao hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kung’oka tena

Spread the loveUWEZEKANO wa Paul Makonda, kuendelea na wadhifa wake wa mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Mabeyo awataje waliotaka kuzuia urais wa Samia

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu...

Habari za SiasaTangulizi

Vilio vyatawala miili ya wanafunzi wanafunzi ikiagwa Arusha

Spread the loveHUZUNI na vilio vimetawala kwa maelfu  ya waombolezaji wakiwemo familia...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

error: Content is protected !!