Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa awafunda Watanzania ughaibuni
Habari za Siasa

Majaliwa awafunda Watanzania ughaibuni

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaoishi ughaibuni kuwa mabalozi wazuri kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi wanazoishi ili kujenga taswira nzuri ya Taifa lao huko waliko. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ameyasema hayo jana tarehe 28 Oktoba, 2022 wakati akizungumza na Watanzania waishio katika Jamhuri ya Korea kwenye ukumbi wa hoteli ya Mondrian iliyopo Seoul nchini humo.

Majaliwa pia amewataka Watanzania hao watumie fursa walizonazo kushawishi na kuvutia uwekezaji nchini Tanzania.

“Tumieni ushawishi na fursa mlizonazo kuwavutia wawekezaji na siku zote semeni mazuri na fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania bila kusahau kuwasemea vizuri viongozi wakuu hasa dhamira nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuliletea maendeleo Taifa.”

Aidha, amewataka wajenge utamaduni wa kutumia lugha ya Kiswahili kama fursa ya kiuchumi kwani nchi nyingi zinahitaji walimu, waandishi, watangazaji na wakalimani wa lugha ya kiswahili.

Pia Majaliwa amewahakikishia kuwa Tanzania ipo salama na Rais Samia anafanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba maisha ya Watanzania yanaimarika kwa kuendelea kusogeza karibu huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo maji, umeme na elimu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Korea, John Bakunda ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuendelea kuimarisha diplomasia ya kiuchumi na mataifa mbalimbali duniani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!