August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majanga ya moto mashuleni yakithiri

Bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Edwaed Lowassa iliyoko wilayani Monduli, Arusha limeteketea kwa moto

Spread the love

SERIKALI imekiri kukithiri kwa majanga ya moto mashuleni na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo, anaandika Dany Tibason.

Akijibu swali bungeni leo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo amesema kwa mwaka 2016 pekee nchi ilikumbwa na majanga ya moto kwenye shule za sekondari 29 zikiwemo mbili zisizo za serikali.

Katika kipindi hichohicho kilichoanzia Januari mpaka Disemba, majanga ya moto yalizikumbua shule mbili za msingi, moja ikiwa ni ya serikali.

Naibu Waziri Jafo amesema matukio ya ajali za moto kwenye shule nchini yaliongezeka kasi kwani kati ya Agosti mosi na 12, shule tano za sekondari ziliungua.

Tatizo kubwa amesema ni kwamba mpaka sasa hakujapatikana uhakika hasa wa chanzo cha matukio hayo mashuleni ni kipi.

Kuna uwezekano kwamba kwa zile shule kongwe, kwa maana ya zilizojengwa miaka mingi nyuma, moto huchangiwa na hitilafu ya umeme inayotokana na uchakavu wa miundombinu. Hujuma pia huweza kuwa sababu, alisema.

Naibu Waziri amesema majanga ya moto mashuleni yanaweza kudhibitiwa ikiwa patakuwa na ushirikiano wa wahusika wote ikiwemo kutambua na kudhibiti viashiria.

Katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu, serikali imeagiza halmashauri nchini kusimamia uundaji wa kamati za kukabiliana na majanga ngazi ya halmashauri na shule.

Alikuwa akijibu swali la Mwantakaje Haji Juma (Bububu), aliyeuliza mpango wa serikali katika kudhibiti ongezeko la majanga ya moto kwenye shule hasa Tanzania Bara.

error: Content is protected !!