Monday , 29 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Majambazi saba yauawa Mwanza
Habari Mchanganyiko

Majambazi saba yauawa Mwanza

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, ACP Jonathan Shanna
Spread the love

WATU saba wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na jeshi la polisi mkoani Mwanza wakati wa majibizano ya kurushiana risasi na askari polisi. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Katika tukio hilo pia jeshi hilo limefanikiwa kukamata silaha mbili ikiwemo moja aina ya AK 47 namba 56 – 3844714 inayodaiwa usajili wake ni wa nchini Burundi.

Silaha nyingine iliyokamatwa katika tukio hilo la ujambazi ambalo ni la tano kwa miezi miwili ya Oktoba na Novemba ni aina ya FN yenye namba 865895 inayodaiwa kutoka pia Burundi ikiwa na magazine moja risasi tano katika maeneo ya mlima uliopo jirani na shule ya msingi Kishiri wilayani Nyamagana.

Majambazi hao wameuwawa baada ya jambazi aliyefahamika kwa majina ya Hashimu Said Abbas mwenye umri wa miaka 48 mkazi wa Shamaliwa kukamatwa na polisi kufuatia kutoroka katika tukio liliotokea Novemba 14 mwaka huu la jambazi.

Jonathan Shanna ni Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza akizungumza katika eneo la tukio hilo amesema majambazi hao wanadaiwa kuhusika na matukio ya uhalifu wa kutumia silaha na kupora fedha na mali za watu katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Mwanza, Mara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Kamanda Shanna amesema pia majambazi hao inadaiwa hufanya matukio ya unyang’anyi kwa kutumia silaha katika wilaya za Bukombe, Chato, Geita, Bunda, Bariadi na Itilima.

“Majambazi hawa ndio waliohusika na mauaji ya mfanyabiashara Richard Slaa wilayani Nyamagana na kama nilivyosema hufanya matukio katika mikoa hiyo,” alisema Shanna

Kwamjibu wa Kamanda alisema, mmoja wa majambazi waliokamatwa aliyefahamika kwa jina la ndiye aliwaeleza askari kuwa ametumwa na wenzake ambao wako katika mapango ya mlima wa shule tajwa hapo juu kwenda kuangalia mazingira ya eneo la kufanyia uhalifu,hususani Buzuruga ambako kuna maduka mengi ya miamala ya fedha

“Baada ya mahojiano ya Polisi na Hashimu alikubali kuwapeleka waliko wenzake na alipofika alitoa sauti ya neno SHEMEJI, ndiyo ilikuwa ishara inayodaiwa kutumiwa na jambazi huyo,hapo ndipo majambazi wenzake walipoanza kuwafyatua risasi askari,” alisema Kamanda Shanna.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza na maelfu ya wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo, amelipongeza jeshi la polisi katika mikoa ya Mwanza na Geita chini ya vikosi maalum vya makachero, kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa.

“Wananchi watambue serikali iko kwajili ya kulinda raia,lakini kuna watu wachache wanao haribu amani na Polisi hawapo kwa ajili ya kuuwa watu na hawapendi lakini inawabidi kufanya hivyo ili kulinda jamii kabla wahalifu hawajafanya madhara makubwa,” alisema Mongella.

Nao wanachi wa kata hiyo ya Kishiri wameiliomba serikali ya mkoa huo kuwajengea kituo kidogo cha polisi,kufuatia kata hiyo kuonekana maficho ya majambazi kutokana na mazingira ya kata hiyo kuwa na mapango mengi yam awe.

“Tatizo linali tukabili katika eneo hili na kupelekea majambazi kufanya maficho ni kuzungukwa na giza kwa kukosa miundombinu ya umeme,barabara kuwa mbovu na ukosefu wa kituo cha polisi maana mpaka twende kwenye kituo cha Nyakato,”Grace Lucas – mkazi wa Kishiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

Habari Mchanganyiko

Kampeni ya Samia Legal Aid yazinduliwa Manyara, kesi 45 zapokelewa

Spread the love  KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, imezinduliwa...

Habari Mchanganyiko

NMB ya kwanza kuzindua Malipo kwa QR na UnionPay International

Spread the loveBENKI ya NMB kwa kushirikiana na UnionPay International (UPI), wamezindua...

error: Content is protected !!