Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa: Vijiji vyote Tanzania kufikiwa na umeme
Habari za Siasa

Majaliwa: Vijiji vyote Tanzania kufikiwa na umeme

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, imedhamiria kufikisha huduma ya umeme katika vijiji vyote nchini vikiwemo na vijiji 25 vya wilaya ya Ruangwa ambavyo bado havijafikiwa na umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kufuatia hatua hiyo, waziri mkuu amewataka wananchi walio katika vijiji ambavyo bado havijaunganishiwa nishati ya umeme wafanye maandalizi kwa sababu maeneo mengine tayari wakandarasi wameshapatikana.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu jana Jumanne, tarehe 23 Juni, 2020 imesema, majaliwa ameyasema hayo wakati alipozungumza na wananchi katika vijiji vya Nanjaru, Nambilanje, Mkaranga, Namichiga na Mbekenyera akiwa kwenye ziara yake ya kikazi wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Pia, Majaliwa ni Mbunge wa Ruangwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema wilaya ya Ruangwa ina jumla ya vijiji 90 kati yake vijiji 25 tu ndio bado havijafikiwa na huduma ya umeme lakini tayari mkandarasi ameshapatikana na ameshaanza kazi, hivyo aliwataka wananchi wajiandae kuunganisha umeme kwenye nyumba zao za makazi na biashara.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

“Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme na amepunguza gharama za kuunganisha umeme kutoka Sh. 380,000 hadi Sh. 27,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama hizo.”

Waziri mkuu alisema licha ya gharama za kuunganishiwa umeme kupunguzwa, pia wananchi hatolazimika kulipia gharama za nguzo pamoja na gharama za fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwani tayari zimeshalipiwa na Serikali.

Vilevile, waziri mkuu alisema, Serikali imeboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kuwa dawa na vifaa tiba vinapatikana katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya na kwamba haitaki kuona mwananchi anakwenda maeneo hayo na kukosa huduma.

“Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alipoingia madarakani aliongeza bajeti ya dawa kutoka Sh. 31 bilioni na kufikia Sh. 269 bilioni, hatutarajii kusikia mgonjwa amekwenda zahanati akaandikiwa cheti na kisha akaelekezwa kwenda kununua dawa kwenye maduka ya watu binafsi.”

Waziri Mkuu amesema ni lazima dawa zipatikane katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya kulingana na hadhi ya eneo husika kama zahanati lazima dawa zinazotakiwa kuwepo kwenye zahanati ziwepo, kadhalika kituo cha afya na hospitali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!