Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaliwa: Tumwombee mama yake Magufuli
Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Tumwombee mama yake Magufuli

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewaomba Watanzania kumwombea Suzana, mama mzazi wa hayati Rais John Pombe Magufuli (61). Anaripoti Regina Mkonde, Dodoma … (endelea).

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo asubuhi Jumatatu tarehe 22 Machi 2021, viwanja vya Bunge jijini Dodoma, wakati wabunge walipokuwa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dk. Magufuli.

Mama yake Dk. Magufuli, ni mgonjwa kwa zaidi ya miaka mitatu na mara kadhaa, mwaane (Dk. Magufuli), alikuwa akiwaeleza Watanzania kumwombea mama yake ili aweze kupona.

Majaliwa amesema, yeye binafsi, anapata wakati mgumu kumwelezea Dk. Magufuli “binafsi inanipa shida kusema mbele yake, naona kama ananipa maelekezo, ananipigia simu, kwa kweli ananipa shida sana.”

Majaliwa Kassim, Waziri Mkuu wa Tanzania akiaga mwili wa Hayati John Magufuli

Akionekana mwenye majonzi, Majaliwa amesema “leo tupo hapa tunamuaga lakini mama yake yuko kitandani, tumwombee mama yake ili apate nguvu.”

Majaliwa amesema “kila mmoja ananamna ya kumwelezea, hata wananchi wameonyesha hilo, tumeona Dar es Salaam kwa siku mbili, tumeona Dodoma jana, kikubwa tumwombee.”

“Huzuni hii si yetu sisi tu, ni maeneo mbalimbali ya Afrika na nje ya Afrika kuwa alikuwa kiongozi wa watu. Leo tumepata fursa ya kuja kumuaga, kwa uzoefu nilioupata Dar es Salaam, wabunge msingeweza kumuaga na ndiyo maana tumeamua kumleta hapa,” amesema Majaliwa.

Majaliwa amesema, kutokana na umati huo, ndiyo maana “tumeamua kubadilisha utaratibu wa kumuaga. Hatuwezi kupita kimwona lakini tutampitisha maeneo mbalimbali.”

Dk. Magufuli, alifikwa na mauti saa 12:00 jioni ya Jumatano tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo.

Mwili wake, unaagwa kitaifa, leo Jumatatu Uwanja wa Jamhuri Dodoma, kesho Zanzibar, keshokutwa itakuwa Mwanza, Alhamisi itakuwa Chato na Ijumaa itakuwa maziko yatakayofanyika nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Tayari imetangazwa leo Jumatatu na Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, ni siku za mapumziko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!