Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa: Tumedhamiria kuboresha miundombinu ya bandari
Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Tumedhamiria kuboresha miundombinu ya bandari

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya bandari ili kuvutia idadi kubwa ya watumiaji zikiwemo nchi za ukanda wa maziwa makuu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ameyasema hayo jana Jumanne, tarehe 20 Julai 2021, alipokutana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho, Mkurugenzi wa Bandari, TASAC, TBS, TMDA, Kamishna wa Forodha pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya usafirishaji.

Alisema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya hatua zilizofikiwa katika uboreshwaji wa huduma mbalimbali bandarini zikiwemo za upakuaji wa mizigo.

Majaliwa alisema, Serikali imejipanga kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mizigo yote inayopitia bandarini inapakuliwa katika kipindi cha muda mfupi.

Alisema bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga zimefanyiwa maboresho makubwa, hivyo amewasisitiza wadau wa sekta binafsi waendelee kuleta meli za kutosha.

Majaliwa alisema mbali na maboresho yaliyofanyika katika bandari hizo, pia bandari za Kabwe, Kasanga nazo zimeboreshwa pamoja na ujenzi wa bandari ya Karema ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria katika nchi za Congo, Zambia na Burundi.

Naye, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Chamuriho alisema, ujenzi ndani ya bandari ya Dar es Salaama unaelekeka kukamilika “Gati zote saba tumezimaliza na sasa tunamalizia eneo la makontena katika gati namba sita na saba ambalo litakamilika Agosti, 2021, hii itasaidia kuongeza ufanisi ndani ya bandari”

Pia, alisema wataendelea kuzingatia masuala yote ya kisheria, kisera, kiutawala na kiutendaji na kuyasimamia kikamilifu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa bandari ili kila anayeitumia aweze kunufaika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Msanja Kadogosa alisema shirika hilo limefanikiwa kukarabati mabehewa zaidi ya 200 ya mizigo ambayo yanaenda nchi za Burundi na Kongo.

Kadogosa alisema katika mwaka huu wa fedha, Serikali imelitengea Shirika hilo bajeti kwa ajili ya kukarabiti mabehewa 660 na kazi ya ukarabati itaanza muda wowote, pia vichwa vingine tisa vitakarabtiwa kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji wa mizigo.

Akizungumzia kuhusu usafirishaji wa mafuta nchini Uganda, Kadogosa alisema wameanza kutekeleza zoezi hilo ambalo lilikwama kwa takribani miaka 15 na wiki ijayo watapeleka lita milioni moja kwenda nchini Uganda.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau wa sekta ya bandari wameipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali inazochukua katika kuboresha sekta hiyo na wameshauri hatua zaidi zichukuliwe ili kuvutia zaidi watumiaji wa bandari nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!