Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa: Tuende tukawatumikie wananchi
Habari za Siasa

Majaliwa: Tuende tukawatumikie wananchi

Spread the love

 

WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amewataka mawaziri walioapishwa leo jijini Dodoma kwenda kuwatumikia wananchi kwa kuwa ndilo jukumu kuu la serikali. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo … (endelea).

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ikulu Chamwino jijini Dodoma katika hafla ya kuwaapisha mawaziri wanne na mwanasheria mkuu wa Serikali walioteuliwa jana na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema anaamini watafanya kazi pamoja huku wakifuata maelekezo ya chama (CCM) ambayo yanalenga kuisaidia serikali kutoa huduma kwa wananchi.

“Tuende tukawatumie wananchi kwenye maeneo yao, kila mmoja anajukumu la kumhudumia mwananchi. Niahidi kwa niaba yao (mawaziri) tutaendelea kuwajibika kwa weledi na uaminifu mkubwa,” amesema.

Mbali na kuwapongeza mawaziri hao, pia amewasihi hao kufanya kazi ipaasavyo katika kila sekta waliyopamgwa kwa uaminifi na kufuata matakwa ya Rais Samia.

Mawaziri hao walioapishwa leo ni Januari Makamba kuwa waziri kuwa waziri wa nishati, Dk. Ashatu Kijaji kuwa waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari, Profesa Makame Mbarawa kuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi, Dk. Stergomena Tax kuwa waziri wa ulinzi.

Wakati Dk. Elieza Feleshi ameapa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Profesa Adelardus Kilangi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!