Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa: Tanzania tutaisaidia Burudi kujiunga SADC kumuenzi Nkurunziza
Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Tanzania tutaisaidia Burudi kujiunga SADC kumuenzi Nkurunziza

Spread the love

TANZANIA imeahidi kuisaidia Burundi ili iweze kujiunga katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Ijumaa tarehe 26 Juni 2020 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika shughuli ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Kurunziza iliyofanyikia Uwanja wa Uwanja wa Mpira wa Ingoma mjini Gitega, Burundi.

Majaliwa amehudhuria kwa niaba ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. Pia, Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mkewe, Salima wamehudhuria shughuli hiyo.

Mwili wa Nkurunziza aliyefariki dunia ghafla tarehe 8 Juni 2020 kwa shinikizo la damu unazikwa leo Ijumaa Mji wa Gitega katikati ya Burundi.

Nkurunziza alifikwa na mauti, ikiwa imesalia miezi miwili kukabidhi madaraka kwa Rais mteule wa wakati huo, Jenerali Evariste Ndayishimiye.

Kutokana na kifo hicho, Jenerali Ndayishimiye aliapishwa tarehe 18 Juni 2020 na leo anaongoza maelefu ya Warundi, wageni mbalimbali wa ndani nan je katika shughuli hiyo ya mwisho kwa mwili wa Nkurunziza.

 Akitoa salamu, Majaliwa ameanza kwa kusema, “niko mbele yangu nikimwakilisha Rais John Pombe Magufuli ambaye angependa kuungana nanyi katika tukio hili kubwa lakini ameshindwa kufika kutokana na majukumu.”

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ukiagwa

“Jambo hili ni kubwa sana, kwa niaba ya Rais Magufuli na Watanzania, tunatoa pole kwako Rais (Jenerali Ndayishimiye)” na Denise, mjane wa Nkurunzinza

Majaliwa ametumia fursa hiyo, kuweleza Warundi wamuunge mkono Rais mpya wan chi hiyo, Jenerali Ndyayishimiye ili aweze kuanza majukumu yake vizuri.

“Nkurunzinza amefanya mambo mengi sana pamoja na kuunganisha nchi hizi mbili kwa kuziunganisha Tanzania na Burundi. Tanzania na Burundi si majirani bali ni ndugu,” amesema

Majaliwa amesema, Nkurunziza kabla ya kufikwa na mauti alizungumza na Mwenyekiti wa SADC, Rais Magufuli “alizungumza akiomba iwe mwanachama wa SADC, nasikitika ametangulia jambo hilo likiwa halijafanikiwa, imani yangu Rais (Ndayishimiye) utalikamilisha.”

“Tanzania tutakusaidia ili kuendeleza hilo aliloliacha na Burundi liingie kwenye SADC. Kwa niaba ya Watanzania na Rais Magufuli nitoe pole tena,” amesema Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!