Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa: Reli ya kimataifa Mtwara- Mbambabay kujengwa
Habari za Siasa

Majaliwa: Reli ya kimataifa Mtwara- Mbambabay kujengwa

Spread the love

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema, Serikali inataka kuanza ujenzi wa reli ya kimataifa ya kutoka Mtwara – Songea – Mbamba Bay yenye matawi huko Mchuchuma na Liganga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

“Upembuzi yakinifu tayari umeshafanyika na michoro yote iko tayari. Na hii iko kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, ibara ya 59 (d),” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana Jumanne, tarehe 20 Oktoba 2020 wakati akizungumza na wakazi wa Ndanda, wilayani Masasi katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Njenga.”

Ibara ya 59 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM inasema: “Katika miaka mitano ijayo, chama kitaielekeza Serikali iendelee kuwekeza katika miundombinu ya kimkakati. Miundombinu hiyo inajumuisha ya reli, viwanja vya ndege na bandari.”

“Pia, kuboresha huduma za usafiri wa anga, baharini na kwenye maziwa kwa kununua vyombo vipya vya usafiri na kukarabati vilivyopo ili kuimarisha huduma….”

Kwenye uk.94 ibara ya 59(d) inafafanua kwamba ili kufikia azma hiyo, katika kipindi hicho, miradi itakayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ni pamoja na ujenzi wa reli ya Mtwara – Songea – Mbamba-bay na matawi ya Liganga na Mchuchuma (km. 1,000).

Majaliwa ambaye yuko mkoani Mtwara kumuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli, alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na mgombea udiwani wa kata ya Njenga, Ester-Stella Kambanga na wagombea udiwani wengine wa CCM.

Akielezea kuhusu sekta ya maji, Mheshimiwa Majaliwa alisema Serikali ilitoa Sh.11.2 bilioni kwa ajili ya miradi ya maji ya Shaurimoyo, Mkalola, Mpitimbi, Shitingi, Sindano na Lihecha.

Akielezea kuhusu uboreshaji wa barabara, Majaliwa alisema ujenzi wa barabara ya Nanganga – Ruangwa kwa kiwango cha lami mkandarasi keshafika site na kazi imeshaanza. Alizitaja barabara nyingine ambazo ziko mbioni kujengwa kuwa ni Masasi – Nachingwea (km.45), Nachingwea – Ruangwa (km. 50) na Nanganga – Masasi (km.45).

Akifafanua kuhusu uboreshaji wa sekta ya elimu, Mheshimiwa Majaliwa alisema sekondari ya Ndanda ni miongoni mwa shule kongwe zinazotupiwa jicho na Serikali na tayari Sh.600 milioni zilishatolewa ili kuanza ukarabati wa bwalo. “Tunataka hii shule irudie kwenye hadhi yake ya zamani,” alisema.

Majaliwa alitoa wito kwa wanafunzi wa Ndanda wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao na Serikali itaendelea kutoa mikopo ya elimu ya juu. “Wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita wana fursa ya kupata mikopo ya kuendelea na elimu ya juu kwani Serikali hii imeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kutoka Sh.348.7 bilioni na sasa hivi tunatoa Sh.464 bilioni.”

Alisema idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaopata mikopo imefikia 130,883 kutoka 98,300 na pia ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini hivi sasa ni 87,813 kutoka 65,064 wa mwaka 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!