Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa: Mradi wa SGR utakamilika kama ulivyopangwa
Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mradi wa SGR utakamilika kama ulivyopangwa

Spread the love

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha mradi huo unajengwa kwa viwango na kukamilika kama ilivyobainishwa kwenye mkataba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri katika vipande vyote na kwamba Serikali itahakikisha mradi huo haukwami na itakabiliana na viashiria vyote vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wake.

Ameyasema hayo leo tarehe 24 Novemba, 2022 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni kuu ya Dodoma katika eneo la Mkonze, jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni hiyo, Majaliwa amewataka Watanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huo wasimamie usalama wa mradi na wawe walinzi ili ukamilike kama ilivyokusudiwa.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassam inaendelea kufanya maboresho kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji.

“Rais Samia anaendelea na mkakati wake wa ujenzi wa reli, endeleeni kuwa na imani na Serikali yenu, lengo lake ni kuhakikisha anainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”

Aidha, Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuwa na mkakati wa maeneo ya uwekezaji kutokana na fursa ya ujenzi wa reli hiyo ikiwemo ujenzi wa kituo cha mabasi jirani na stesheni hiyo.

Kwa upande wake, Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa Shirika hilo lipo kwenye mpango wa ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ya mizigo. “Hadi sasa TRC imesaini mkataba wa ununuzi wa vichwa vya treni vya umeme 19, seti za treni 10 zenye uniti 80.”

Amesema pia shirika hilo itanunua mabehewa ya kawaida ya abiria 89, mabehewa ya ghorofa 30 ambayo yanakuja, mabehewa ya mizigo 1,430 na vifaa vya matengenezo 26.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!