May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa: Madaktari endeleeni kumhudumia Mama yake Magufuli

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, madaktari wanaomhudumia Suzana, mama mzazi wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, wataendelea na jukumu hilo hadi mwisho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato…(endelea)

Majaliwa amesema, mama mzazi wa Hayati Magufuli, amekuwa mgonjwa kwa zaidi ya miaka miwili na Rais mpya wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo aendelee kuhudumiwa.

“Mama mzazi wa mpendwa wetu Dk. John Pombe Magufuli, yuko kitandani kwa zaidi ya miaka na maagizo yako mheshimiwa Rais, tunawataka madaktari kuendelea kumhudumia hadi atakaporudi kwenye uimara wa afya yake,” amesema Majaliwa

Dk. Magufuli alifariki dunia Jumatano ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na unazikwa leo Ijumaa 26 Machi 2021, nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

error: Content is protected !!