Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa maagizo kambi ya wakimbizi Tanganyika
Habari za Siasa

Majaliwa maagizo kambi ya wakimbizi Tanganyika

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wakazi wanaoishi katika makazi ya wakimbizi ya Mishamo Wilayani Tanganyika kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao kwa kutoa taarifa za watu wanaoingia eneo hilo kutoka nchini bila kufuata utaratibu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Katavi … (endelea).

Amesema eneo hilo limekuwa kimbilio la wahalifu wakiwemo wezi na wawindaji haramu hivyo amewasihi wakazi hao kusimamia ulinzi na usalama.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana Alhamisi, tarehe 26 Agosti 2021, alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi. Amesema Serikali haifurahii kuona wakazi wa maeneo hayo wanaruhusu watu wasiokuwa na vibali kuingia katika eneo hilo.

“Ninawaomba msimamie usalama katika eneo hili, Mshiriki kuzuia wenzenu wanaokuja kutoka nchi jirani hata kama ni ndugu zenu, kama hajaingia kwa kufuata utaratibu toa taarifa kwa Mkuu wa Makazi, lazima tushirikiane kuifanya nchi hii kuendelea kuwa na historia yake ya Amani na utilivu.”

Aidha, katika kuhakikisha wanasimamia suala la ulinzi na usalama, Waziri Mkuu amewataka wakazi hao watumie vikao vyao vya kijamii kukemea vitendo vya kihalifu na waelimishane juu ya umuhimu wa kulinda na kudumisha amani. Pia wahamasishane kufuata taratibu wakati wanapotoka na kuingia katika makazi hayo.

Awali, Majaliwa alitembelea kituo cha afya Mishano ambacho Serikali ilitoa Sh.400 milioni ili kufanya maboresho na sasa kituo hicho kimejenga chumba cha upasuaji na wodi ya mama na watoto na amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuboresha miundombinu ya huduma za Afya katika maeneo yote nchini.

Akizungumzia maboresho ya kituo hicho ambacho pia kina uwezo wa kutoa huduma ya upasuaji wa dharula kwa akina mama, Mkazi wa Kijiji cha Mishamo, Stella Jonasi amesema awali kina mama walikuwa wanahangaika kwa kukosa sehemu ya kujifungulia hivyo kuwalazimu kusafiri kwa umbali mrefu hadi mpanda kufuata huduma hiyo.

Naye Emmanuel Kijumba, Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha Kituo hicho pamoja na kuongeza idadi ya Madaktari, wauguzi na kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!