October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa azuru kaburi la Hayati Magufuli Chato

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezuru kaburi la Hayati John Pombe Magufuli na kushiriki sala ya kumwombea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Ametembelea kaburi hilo jana Jumanne, tarehe 12 Oktoba 2021, nyumbani kwa hayati, Chato mkoani Geita.

Hayati Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania, alifikwa na mauti saa 12 jioni ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho, Dar es Salaam.

Mwili wa Hayati Magufuli, ulizikwa nyumbani hapo tarehe 26 Machi 2021.

Majaliwa alifika nyumbani hapo na kupokelewa na Mama Janeth, Mjane wa Hayati Magufuli kisha kushiriki sala fupi ya kumwombea kiongozi huyo aliyefikwa na mauti akiwa madarakani.

Majaliwa aliambatana na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

error: Content is protected !!