Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa azungumzia tatizo la maji Tanzania
Habari za Siasa

Majaliwa azungumzia tatizo la maji Tanzania

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote nchini vikiwemo na vya wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Amesema suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali katika awamu hii, hivyo suala la upatikanaji wa huduma ya maji ni endelevu.

“Tutaendelea kuboresha miradi ya maji ili maeneo yote nchini yapate maji ya uhakika,” amesema Majaliwa

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, tarehe 23 Julai 2021, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Mpara, Mtimbo, Mmawa, Chikoko, Chinokole na Kilimahewa wilayani Ruangwa.

Majaliwa amesema, Serikali inatekeleza kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani ili kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma hiyo karibu na maeneo yao ya makazi. Amewataka waendelee kuiamini Serikali yao kwa sababu imedhamiria kuwatumikia.

Akizungumzia kuhusu tatizo la maji wilayani Ruangwa amesema Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa maji wa Mbwinji ambao unatoa maji Ndanda hadi Ruangwa. “Mradi huu mkubwa unatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la upatikanaji wa maji wilayani Ruangwa.”

Waziri Mkuu amesema mbali na huduma ya maji safi na salama, pia Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini, hivyo amewataka wananchi wafanye maandalizi ya kufikisha nishati hiyo katika makazi yao.

Amesema Rais Samia anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme nchi nzima vikiwemo na vijiji vya wilaya ya Ruangwa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni Sh. 27,000 tu.

Pia, Majaliwa amesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zote zimeshabebwa na Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!