December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa azindua safari za treni ya mizigo Tanga-Moshi

Spread the love

KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezindua safari za treni za mizigo kutoka Mkoa wa Tanga kuelekea Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 20 Julai 2019 katika viwanja vya Stesheni ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Majaliwa amesema utekelezaji wa urejeshaji huduma ya usafiri wa reli nchini, ni muendelezo wa jitihada za serikali katika kufikisha huduma muhimu kwa jamii.

Majaliwa amesema serikali itaanzisha usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar es Salaam, Moshi hadi Arusha.

“Tunaendelea kuboresha miundombinu ya reli ili kuifungamanisha na sekta nyingine, ndiyo maana tumewekeza katika ujenzi wa reli ya kisasa na ukarabati wa reli ya kati. Tutaanzisha Usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar-Moshi-Arusha,” amesema Majaliwa.

Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) amesema serikali imetumia Sh. 5.7 bilioni kuirudisha njia hiyo, iliyofungwa kwa miaka 12.

“Mpaka sasa tumetumia Sh. 5. 7 bilioni kuirudisha njia hii, na wahandisi wazawa ndio wamesimamia zoezi hili lote,” amesema Kadogosa.

error: Content is protected !!