May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa azindua ofisi za polisi zenye thamani ya Sh bilioni 1.3

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2021 amefungua majengo ya Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Singida na Ofisi za Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Singida, miradi ambayo imegharimu shilingi bilioni 1.314. Anaripoti Hellena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Waziri Mkuu amesema kuwa amefurahishwa na mradi huo ambao ujenzi wake umetumia muda mfupi na umeokoa kiasi kikubwa cha fedha za Serikali.

Ameahidi kuwa serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya vyombo vya ulinzi na usalama.

“Nawapongeza sana wasimamizi wa mradi huu kwa kuhakikisha unatekelezwa vema na kuakisi thamani ya fedha za mradi yaani value for money sanjari na kukamilika kwa wakati. Tumeelezwa hapa kuwa mradi huu uliotekelezwa kwa mfumo wa nguvu kazi yaani force account, ulianza tarehe 20 Februari, 2021 na kumalizika tarehe 15 Julai 2021 na kwa gharama ya shilingi bilioni 1.3 badala ya ile ya mkandarasi ya 1.9.”

Aidha, Waziri Mkuu amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kufuata miongozo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya kazi kwa weledi na kuboresha mifumo ya kiutendaji wa jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo vingine ili kuepuka ucheleweshwaji wa upelelezi wa kesi kwa lengo la kuondoa mlundikano wa mahabusu magerezani.

“Naliagiza Jeshi la polisi liendelee kuimarisha mfumo wa ulinzi na usalama kwenye ngazi ya jamii ili kujenga mfumo wa kutambua, kutoa taarifa na kuchukua hatua za awali dhidi ya vihatarishi vya ulinzi na usalama vinavyojitokeza katika maeneo yao.

Aidha, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Chilo, amesema Wizara yake iko thabiti katika kusimamia Sheria na wako tayari kuhakikisha raia wote na mali zao wanaishi kwa usalama na utulivu na kutoa wito kwa watu wote wanaopanga kufanya matendo ya kiuhalifu kuacha mara moja.

Wakati, Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro  amesema ujenzi huo umekamilika kwa kipindi cha miezi mitano kwa kutumia mfumo wa nguvu kazi, (Force Account) ambapo jengo hilo lina ghorofa mbili, vyumba vya ofisi 30 na kumbi mbili za mikutano.

error: Content is protected !!