October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa aziagiza wizara, halmashauri ziimarishe mazingira uchumi shirikishi

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameziagiza wizara, halmashauri na taasisi za Serikali na binafsi, ziimarishe mazingira ya uchumi shirikishi ili kukuza kipato cha wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 4 Oktoba 2021, katika kongamano la tano la kitaifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, lililofanyika jijini Dodoma.

“Naagiza wizara za kisekta na uchumi ziimarishe kiumdombinu muhimu kama ya kilimo, uvuvi, mifugo, biashara na uwekezaji, ili kukuza ajira na kipato cha mtu mmoja mmoja. Halamshauri zihakikishe hafua za uwezeshaji wananchi kiuchumi zinatenegwa bajeti na kuwajengea uwezo maafisa biashara,” amesema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Majaliwa ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango, izisimamie taasisi za fedha ili zitoe huduma za kifedha, ikiwemo mitaji kwa masharti nafuu hasa kwenye maeneo ya vijijini na pembezoni mwa nchi.

Waziri Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuimarisha mazingira ya ukuzaji uchumi jumuishi na kuvutia uwekezaji, kwa lengo la kupanua shughuli hizo.

Wakati huo huo, Waziri Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa nchini, kwa kushirikiana na wafanyabiashara ndogondogo, ikiwemo wamachinga, kutenga maeneo mazuri ya ufanyaji biashara zao, ambayo itakuwa rahisi wananchi kuyafikia.

error: Content is protected !!