December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa awashauri walioshindwa udiwani, ubunge

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewashauri wagombea wasioridhika na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 kufuata taratibu za kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Majaliwa ametoa ushauri huo jana Alhamisi tarehe 29 Oktoba 2020 katika Baraza la Maulid ya Mtume Muhammad, lililoandaliwa na Taasisi ya Nida Textile lililofanyioa Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alisema wagombea kuwa na uvumilivu katika kipindi cha utangazwaji wa matokeo ya uchaguzi huo ambao unaonyesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejizolea madiwani na wabunge wengi.

“Hivi sasa zoezi la kutangaza washindi linaendelela. Hivyo, katika kipindi hiki nitoe rai kwa vyama vya siasa, wagombea na wafuasi wa wagombea kila mdau anayeitakia kheri kuwa na nguvu na subira wakati matokeo hayo yanatolewa. Ikitokea kutoridhika na matanagzo hayo ni vyema taratibu za msingi zifuatwe,” alisema Majaliwa.

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Waziri mkuu huyo aliwataka Watanzania kuienzi tunu ya amani.

“Nawakumbusha kuenzi tunu ya amani, upendo na umoja hususan kipindi hiki na baada ya uchguzi uliofanywa  na utaratibu wa matokeo unaendelea,” alisema Majaliwa.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo kutoka Taasisi ya NIDA Textile, Saleh Omar, alisema, wameandaa maadhimisho hayo ili kuwakutanisha waumini wa Kiislamu ili kusherekea sikukuu hiyo.

Omar alisema, wameandaa maadhimisho hayo ili kuwapa mawaidha Waislamu kuhusu mafundisho ya Mtume Muhammad.

“Taasisi ya Nida Textile iliona tukiwa tunaadhimisha kuzaliwa kwake Mtume Muhammad  haipaswi kupita bila kupata mafunzo yake, ametuachia sisi wafuasi wake. Kikubwa kuenzi umoja, amani, upendo na mshikamano,” amesema Omar.

error: Content is protected !!