Saturday , 4 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa awapa neno wasio na ajira
Habari za Siasa

Majaliwa awapa neno wasio na ajira

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewashauri wananchi wasiokuwa na ajira kujikita katika masuala ya kilimo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Majaliwa ametoa ushauri huo leo Jumamosi tarehe 5 Desemba 2020, wakati akifungua kongamano la uwekezaji na biashara ya mazao ya biashara, lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo, limeratibiwa na Taasisi inayoshughulika na kilimo cha mbogamboga na matunda (TAHA).

Majaliwa amesema, ili Tanzania ifike katika dira yake ya maendeleo, inatakiwa kila mmoja afanye kazi na kwamba sekta pekee inayotoa fursa nyingi za ajira ni kilimo chenye tija.

“Ili kuifikisha Tanzania tunakotarajia, itatokana na kila mmoja kufanya kazi na fursa ya kilimo imefungua milango, kwa yeyote anayeamua kufanya kilimo kitaalamu na kuzalisha zaidi, ukitaka fedha ya uhakika nenda shambani,” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amesema, kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, ya ‘hapa kazi tu’ imesaidia wananchi wengi kuachana na mambo yasiyo na tija na kujikita katika kufanya kazi.

“Kauli mbiu yetu ya hapa kazi, imesaidia sana kila mmoja kauchana na mambo ambayo hayana tija na kushiriki katika mambo yenye tija kwa kufanya kazi,” amesema Majaliwa.

Waziri mkuu huyo amesema, Serikali imedhamiria kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo kupitia Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya 2020/25 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa mazao, upatikanaji wa pembejeo pamoja na kuwapelekea maafisa ugani kwa wakulima.

“Serikali inafahamu changamoto ya usafirishaji bidhaa na imeweka mikakati kuboresha miundombinu nchini, kwa kufanya ifuatavyo, kwanza ilani yetu imeweka bayana uwekaji mpango wa kuboresha miundombinu ya usafirishaji.”

“Kwa bidhaa zinazoharibika haraka kwa kununua ndege za mizigo kwa kuzingatia mahitaji ya biashara na ukuaji w a uchumi hapa nchini,” amesema Waziri Majaliwa.

Katika kuboresha sekta ya kilimo, Majaliwa amesema, Serikali itanunua ndege mbili za masafa marefu na mbili za masafa ya kati ili kuongeza fursa za biashara nje ya nchi.

Wakati huo huo, Majaliwa ameagiza Wizara ya Kilimo kuanzisha mamlaka itakayosimamia zao la mbogamboga na matunda, pamoja na kituo cha utafiti wa mazao hayo.

Pia, Majaliwa amesema, Serikali imeunda kamati maalumu inayohusisha wataalamu wake na wa sekta binafsi, kwa ajili ya kuainisha changamoto za mifumo ya usafirishaji mazao katika bandari na viwanja vya ndege, kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

“Kufuatia uundwaji huo, napenda kuziagiza taasisi za usafirishaji mizigo hasa anga na bandari kufanyia kazi kwa haraka mapendekezo ya wataalamu kutokana na utafiti wa uboreshaji miundombinu ya usafirishaji, ili kuboresha namna nzuri usafirishaji kufikia masoko,” ameagiza Majaliwa.

Majaliwa amamewaagiza mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kutafuta wawekezaji huku akiwahakikisha Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.

Hali kadhalika, Majaliwa amewaagiza maafisa wa wizara ya kilimo kuzungumza na mabalozi wa nchi za nje waliopo Tanzania, ili kuwaonesha fursa zilizopo nchini kwa ajili ya kupata masoko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!