Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Majaliwa awapa maagizo mameya, wenyeviti wa h’shauri
HabariKitaifa

Majaliwa awapa maagizo mameya, wenyeviti wa h’shauri

Spread the love

WAZIRI MKUU wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri wasimamie ipasavyo matumizi ya fedha zilizokusanywa na zile zinazotoka Serikali Kuu na wahakikishe zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 28 Juni 2022, wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri wa Tanzania Bara katika ukumbi wa Mabeyo Complex jijini Dodoma. Amesema lazima viongozi wajue fedha zinazoingia na maelekezo yake.

Amesema Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kila mwaka inaibua makosa yale yale ikiwamo kuhamisha fedha kutoka fungu moja kwenda jingine bila kufuata taratibu zilizowekwa na kufanyika kwa malipo bila ya kuwepo maelezo au vielelezo.

“Fedha za makusanyo kutumika kabla ya kupelekwa benki. Lazima muhoji kwa nini na mjue hilo haraka. Pia mjiridhishe pale wanaposema hakuna mtandao je ni kweli hakukuwa na mtandao. Fuatilieni na ununuzi wa vifaa hewa hasa kipindi hiki cha ujenzi wa miradi.”

“Viongozi wote mlioshiriki mafunzo mkasimamie vema utawala bora na utawala wa sheria ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa utatuzi wa migogoro sambamba na ushirikishaji wananchi katika maamuzi na mipango ya maendeleo.”

Majaliwa amesema viongozi wote wanatakiwa wahakikishe wananchi wanapata taarifa za utekelezaji wa mipango na bajeti za kutekeleza mipango hiyo. “Utoaji wa taarifa za mapato na matumizi ni muhimu katika kujenga imani kwa wananchi.”

Waziri Mkuu amewataka viongozi hao waimarishe usimamizi wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kazi zinazofanywa zilingane na fedha inayotumika. “Kasimamieni viwango vya ubora wa miradi inayotekelezwa na utekelezaji wa makubaliano yaliopo kwenye mikataba.”

Kwa uapnde wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Innocent Bashungwa amesema mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mameya wa Halmashauri za Majiji na Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya na Miji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!