August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa awapa kibarua watendaji Songwe

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Spread the love

VIONGOZI wa mkoa wa Songwe wametakiwa kushiriki kikamilifu kutatua migogogro ya ardhi ili kuzuia migogoro kati ya wakulima na wafugaji inayohatarisha usalama wa maisha yao, anandika Mwandishi Wetu.

Kauli hiyo ilitolewa siku za hivi karibuni na Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa,wakati wa kikao cha tadhimini kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule za Nanyara alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri zote mkoani Songwe.

Alisema ili kudhibiti migogoro hiyo serikali imeweka utaratibu wa kuweka alama (nembo) mifugo yete na kwamba kila wilaya mkoani humo iwe na nembo yake ili ikitokea mifugo imekwenda wilaya nyingine itambulike kirahisi ili kuzuia wizi na upotevu.

Majaliwa alisisitiza kuwa wafugaji wanatakiwa kufuga mifugo wanayoweza kuimudu na kama mfugaji ana mifugo mingi ni bora apunguze kwa kuiuza ili fedha anayoipata itumike kuboresha makazi na kusomesha watoto shule za msingi, sekondari hadi vyuo vikuu

Hata hivyo,  majaliwa alisema serikali inatakiwa kutenga maeneo ya wafugaji ili waweze kulisha mifugo yao kwa ukosefu wa maeneo ya wafugaji ndiyo chanzo cha kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima yaliyopo shambani.

Alisema kwa upande wa chakula mwaka jana hali ilikuwa mbaya,  lakini mwaka huu kila mtu alimuomba mungu na kuongeza nguvu katika uzalishaji kwa kulima mazao mengi na hatimaye mavuno yamepatikana.

Aliongeza kuwa kumekuwa na tabia ya wakulima kuuza mazao yote na wengine wamekuwa wakinunua na kupeleka nje kwa kudhibiti hali ya njaa.

error: Content is protected !!