Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Majaliwa awaonya waamuzi mpira wa Miguu
MichezoTangulizi

Majaliwa awaonya waamuzi mpira wa Miguu

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka waamuzi watakaochezesha mashindano ya mpira wa miguu ya jimbo la Ruangwa wawe makini na wajiepushe na vitendo vya rushwa. Anaripoti Damas Ndelema/ TUDARCo

Majaliwa ameyasema hayo, leo Agosti 19, 2021 Ruangwa, mkoani Lindi wakati alipokuwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu nane zilizofikia hatua ya robo fainali.

Mashindano yalihusisha timu 38 kutoka katika jimbo hilo na timu hizo nane zimepata zilipata jezi na mpira mmoja kwa kila timu na fainali zitachezwa Agosti 30, 2021.

Waziri Mkuu huyo alisema kuwa waamuzi hao wasiingize maslai yao binafsi kwa kuwa wanataka michezo hiyo ichezwe kwa jitihada za wachezaji wenyewe.

“Waamuzi msiingize maslahi binafsi wala msijiingize kwenye rushwa kutoka timu yoyote, tunahitaji michezo hii ichezwe kwa jitihada za wachezaji wenyewe.” Alisema Majaliwa

Aidha aliendelea kwa kusema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwahamasisha vijana wanaopenda mpira wa miguu waweze kucheza kwa bidii na kuongeza tija. Amesema kwa sasa mpira wa miguu ni ajira na amewataka vijana jimboni humo kuacha uzembe bali wajitume kupandisha viwango vyao.

“Vijana wa Ruangwa jengeni wivu na mjitume sana ili muweze kupandisha viwango vyenu vya uchezaji na hatimaye muweze kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vinavyoshiriki ligi kuu.”

Amewataka viongozi Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Ruangwa (RUDIFA) wasimamie vizuri mashindano hayo ili kuwawezesha vijana wanaoshiriki waweze kutimiza malengo yao.

Waziri Mkuu amesema mbali na kuleta afya na ajira kwa washiriki michezo pia ina tabia ya kuwaunga watu pamoja na kuwawezesha kujadili shughuli za maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!