Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaliwa atoa siku 41 taasisi za serikali zinazodaiwa na vyombo vya habari kuwalipa
Habari Mchanganyiko

Majaliwa atoa siku 41 taasisi za serikali zinazodaiwa na vyombo vya habari kuwalipa

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameziagiza wizara, taasisi na mashirika ya umma yanayodaiwa na vyombo vya habari, hadi tarehe 30 Juni 2021, yalipe madeni hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo leo Alhamisi, tarehe 20 Mei 2021, katika Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), uliofanyika mkoani Morogoro. Kuanzia leo. Hadi 30 Juni 2021 ni sawa na siku 41.

“Najua kuna maelezo tunadaiwa, nitoe maelekezo kwa tasisi zinazodaiwa na vyombo vya habari walipe madeni yao haraka sana, walipe madeni kabla ya tarehe 30 Juni 2021,” amesema Majaliwa.

Katika utekelezwaji wa agizo hilo, Majaliwa ameviagiza vyombo vya habari vinavyodai, kuorodhesha kiasi cha madeni hayo, ili Serikali ifanye utaratibu wa kulipa, kabla ya mwisho wa utekelezwaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021.

“Ili kukazia hili, kama kuna chombo kinaidai wizara au taasisi yoyote ya serikali, iwe mkuu wa mkoa, wilaya, au mkuregenzi anadaiwa kwa kazi halali mliyoifanya, nipatieni hiyo orodha halafu tushughulike nayo,” amesema Waziri Majaliwa .

Waziri Mkuu huyo amesema “huu ni wakati mzuri sana, tunakwenda kuhitimisha bunge la bajeti mwezi ujao, wizara nyingi zimeweka bajeti zinakoma tarehe 30 Juni, mkileta orodha nina hakika mpaka tarehe 30 mmeshalipwa. Hii naamini tumelileta vizuri.”

Katika kipindi cha miaka mitano mfululizo, baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania vimekuwa vikilalamika kuhusu ukata, huku ikitaja sababu zake kuwa ni malimbikizo ya madeni serikalini pamoja na kukosa matangazo.

Kuhusu changamoto hiyo, Waziri Majaliwa ameagiza taasisi za Serikali na wizara kutoa matangazo hayo bila ubaguzi.

 

“Katika lisala yenu, mmezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo hali ngumu ya uchumi, na nafahamu mara kadhaa mmelalamika mnanyimwa matangazo katika taasisi za serikali,” amesema Majaliwa na kuongeza:

“Wakati mwingine huwa mna kile mnachosema maelekezo yametolewa, chombo kingine kisipate habari, nataka niwaambie suala la maelekezo halipo ndani ya serikali na wala halijawhai kutokea.”

Awali, Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alisema, takriban miaka minne iliyopita, sekta ya habari imepita katika wakati mgumu na kusababisha vyombo vya habari kuyumba kutokana na sababu na mazingira.

Amesema, katika miaka ya karibuni, hali ya uchumi katika vyombo vyetu vya habari
imekuwa mbaya kiasi cha baadhi ya vyombo hivyo kusitisha uzalishaji, hivyo kusababisha waandishi wa habari na wahariri kukosa kazi.

“Kimsingi vyombo vyetu huendeshwa kwa matangazo na hapa nchini
serikali ndiye mtangazaji mkuu. Hata hivyo, vyombo vyetu vingi vimejikuta vikishindwa kumudu gharama za uendeshaji kutokana na kupungua kwa matangazo kutoka serikalini, ambapo hata yale machache yanayopatikana hayalipwi kwa wakati,” alisema Balile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!