Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaliwa atoa maagizo kwa wazazi, walezi
Habari Mchanganyiko

Majaliwa atoa maagizo kwa wazazi, walezi

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewataka wazazi na walezi wahakikishe wanawapunguzia watoto majukumu ya nyumbani na kuwawezesha kupata muda wa kujisomea na kupumzika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ameyasema hayo hayo leo Jumanne, tarehe 23 Februari 2021, wakati akizungumza na walimu, wanafunzi na wazazi baada ya kukagua miundombinu ya shule ya Msingi Mitope, Ruangwa.

Majaliwa amesema, iwapo watoto watapata muda mzuri wa kujisomea na kupumzika itawasaidia katika kuwaongezea ufaulu kwenye masomo yao na kutimiza ndoto zao kielimu.

Pia, amewataka wazazi na walezi, wahakikishe wanafunzi wananunuliwa vifaa vyote vinavyohitajika shuleni kama sare, madaftari pamoja na kufuatilia mienendo yao kielimu.

”Wazazi tufuatilie na kujiridhisha kama watoto wetu wanafika shule na kuingia madarasani. Pia tuwe tunakagua madaftari yao na pale tunapoona hawafanyi vizuri tuwasiliane na walimu.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amesema atahakikisha anashirikiana na viongozi wenzake kuendelea kusimamia vizuri shughuli za maendeleo.

Kadhalika, mkuu huyo wa wilaya ameahidi kuendelea kusimamia vizuri fedha zote za maendeleo zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya wilaya ya Ruangwa ili zitumike ipasavyo.

Awali, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mitope, Margareth Mselewa alisema walimu wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafunzi wote wa darasa la saba wanafaulu kwa asilimia 99.

Mwalimu huyo alisema katika matokeo ya mitihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka jana shule yao ilikuwa na jumla ya wanafunzi 21 ambao wote walifaulu na kwenda sekondari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!