Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Mkuu Majaliwa atoa maagizo kwa mkandarasi, Polisi, TRA na Uhamiaji
Habari za Siasa

Waziri Mkuu Majaliwa atoa maagizo kwa mkandarasi, Polisi, TRA na Uhamiaji

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakati wa Tanzanyika baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari ya Kasanga wilayani Tanganyika
Spread the love

KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania, ameiagiza Kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group inayojenga  Bandari ya Karema kwa gharama za zaidi ya Sh.47 bilioni ifanye kazi usiku na mchana na  kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Congo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Katavi … (endelea).

Pia, Majaliwa ametoa muda wa siku 21 kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Polisi, Wizara ya Madini wawe wameanza kutoa huduma katika eneo la Ikola ili kuhudumia wageni wanaotoka Congo.

Taarifa ya ofisi ya waziri mkuu imesema, Majaliwa alitoa agizo hilo jana jioni Jumamosi, tarehe 4 Julai 2020 baada ya kuweka jiwe la msingi la  ujenzi wa Bandari ya Karema inayojengwa ziwa Tanganyika katika kata ya Karema wilayani Tanganyika, Katavi.

Alisema mkandarasi anatakiwa ahakikishe mradi huo unakamilika haraka.

         Soma zaidi:-

Waziri mkuu alisema, mradi huo unalenga kuongeza tija katika shughuli za kibandari kwenye ukanda wa Ziwa Tanganyika ndani na nje ya nchi na kwamba utaongeza fursa za kibiashara nchini na pia utakuwa chachu ya kukuza uchumi pamoja na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi.

“Tumeamua kujenga bandari hii ambayo itawezesha meli zaidi ya moja kupakia na kushusha abiria na mizigo kwa wakati mmoja.”

“Hii ni Serikali ya kuahidi na kutekeleza na ni Serikali ya kusikia na kutenda na ndio maana halisi ya falsafa ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa bandari ya Kasanga wilayani Tanganyika

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Baraka Mdima alisema, mradi huo unahusisha ujenzi wa gati kubwa la kufungia meli lenye urefu wa mita 150 pamoja na kingo ya kuzuia mawimbi makali, uchimbaji wa kuongeza kina cha lango la kuingilia bandarini na sehemu ya kugeuzia meli.

Alisema eneo jinguine ni ujenzi wa miundombinu ya bandari ikiwemo mgahawa, jengo la kupumzikia abiria, majengo ya ofisi, eneo la sakafu ngumu kwa ajili ya kuhifadhia makasha pamoja na miundombinu ya Zimamoto na Tehama. Mradi huo utazingatia ujumuishi wa Reli ya Kisasa (SGR).

“Mradi unajengwa kwa miezi 24 na kukamilika kwa bandari ya kisasa ya Karema, kutaboresha shughuli za kiuchumi katika mkoa wa Katavi na Tanzania kama kusafirisha watu na bidhaa katika maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na nchi jirani za Congo, Burundi na Zambia.”

Kadhalika, waziri mkuu alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera aendelee na operesheni ya kuwasaka watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wa ujenzi wa bandari ya Kasanga wilayani Tanganyika

“Watu wote wanaomiliki silaha bila ya kuwa na vibali watafuwe popote walipo na wachukuliwe hatua za kisheria,” alisema

Awali, waziri mkuu alizungumzia upatikanaji wa umeme katika wilaya ya Tanganyika, alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imedhamiria kufikisha huduma ya umeme katika vijiji vyote nchini, hivyo waendelee kuwa na subira.

“Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme na amepunguza gharama za kuunganisha umeme kutoka Sh. 380,000 hadi Sh. 27,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama hizo,” alisema

Waziri mkuu aliongeza licha ya gharama za kuunganishiwa umeme kupunguzwa, pia wananchi hatolazimika kulipia gharama za nguzo pamoja na gharama za fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwani tayari zimeshalipiwa na Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!