Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa atembelea Banda la NMB, atoa maagizo
Habari Mchanganyiko

Majaliwa atembelea Banda la NMB, atoa maagizo

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezielekeza halmashauri zote za wilaya na miji, kwenye maeneo yenye madini ziandae sheria ndogo (by-laws) kwa kushirikiana na wadau katika sekta ya madini ili ziendane na Sheria ya madini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

 Majaliwa alitoa maagizo hayo jana Jumanne tarehe 9 Mei 2023, wakati akifungua Kongamano la Wachimbaji  Madini na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa(kulia) akifurahia jambo na Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara wa Benki ya NMB David Lugangira(kushoto) alipotembelea Banda la Benki hiyo wakati wa ufungaji wa maonesho ya wiki ya Madini jijini Mwanza. katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima.

 Majaliwa kabla ya kuzungumza, alitembelea matanda mbalimbali likiwemo la Benki ya NMB akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Adam Malima ambapo alizungumza na Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, David Lugangira.

 Katika hotuba yake Majaliwa aliwataka,“wakurugenzi wa Halmashauri wekeni mifumo bora ya kuweka tozo hizo na kuondoa kero kwa wachimbaji wadogo, punguzeni utitiri wa tozo kwa kubuni vyanzo vingine mapato.”

 Alisema Serikali inaendelea na jitihada za kuweka mazingira bora katika sekta ya uchimbaji mdogo na tayari imeshaanza kufanya marekebisho ya baadhi ya Kanuni na Sheria ya Madini na kuboresha mazingira ya biashara.

 “Lengo la kufanya haya yote ni kuwezesha wananchi hasa wachimbaji wadogo nchini na wadau mbalimbali kushiriki ipasavyo katika uchumi wa madini,” alisema.

Akizungumza kuhusu mchango wa Sekta ya madini kwenye pato la Taifa Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa umeongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017, hadi asilimia 7.2 mwaka 2021. “Pia katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 mchango wa sekta ya madini ni asilimia 9.6”

 Amesema kuwa Serikali kupitia sekta ya madini imeweza kukusanya shilingi bilioni 409.66 sawa na asilimia 85.43 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni 479.51 katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2022/2023.

 Pia Majaliwa aliagiza Wizara ya madini kuharakisha mchakato wa kutafuta ufumbuzi wa suala Madini ya Lithium mapema iwezekanavyo ili kuweka wazi viwango vya uongezaji thamani kwa madini hayo kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

 Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kurasimisha maeneo yenye milipuko ya madini ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023 zimetolewa jumla ya leseni 6,381, zikiwemo leseni 3,865 za uchimbaji mdogo wa madini (PML), leseni 1,649 za biashara ndogo ya madini (Brokers).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!