May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa ataka mikakati kuitangaza Serengeti

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Spread the love

 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara na Wwatendaji katika Sekta ya Utalii waweke mikakati ya kuitangaza Mbuga ya Serengeti, ili kuwavutia watalii wa kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Waziri Majaliwa alitoa agizo hilo jana Ijumaa, tarehe 28 Mei 2021, akizindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mara, katika Ukumbi wa Bishop Rudin uliopo kwenye viwanja vya Mwembeni mjini Musoma.

Waziri Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Robert Gabriel, ahakikishe watendaji wake wanatekeleza majukumu yao kwa uweledi katika kutekeleza agizo hilo.

“Mkuu wa Mkoa hakikisha watendaji wote wa mkoa, wanausoma na kuuelewa ipasavyo mwongozo huu. Hakikisha watendaji wako wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uaminifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,” alisema Waziri Majaliwa.

Mbali na uwekaji mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Mara, Waziri Majaliwa aliiagiza Wizara ya Uwekezaji, ishirikiane na mkoa huo ili kukiwezesha Kituo cha Uwekezaji cha Kanda (TIC), kilichopo mkoani Mwanza, kianzishe Kituo cha Kutolea Huduma kwa Pamoja (One Stop Centre) mkoani humo.

“Watu wote muhimu wanaopaswa kutoa huduma katika kituo wawepo, wakiwemo wataalamu wa ardhi, biashara, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), Wakala wa Vipimo, NEMC, Bodi ya Nyama na Bodi ya Maziwa,” alisema Waziri Majaliwa.

Pia, Waziri Majaliwa aliziagiza idara za kisekta kuanzia ngazi ya mikoa na wilaya, zishirikiane katika kubuni njia rahisi zitakazosaidia kuondoa urasimu, ili kurahisisha uwekezaji katika maeneo yao kwa ajili ya kuongeza ajira na vyanzo vya mapato ya Serikali.

error: Content is protected !!