September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa ataja muarobaini migogoro ya wafugaji, wakulima

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameagiza Serikali za Vijiji zitenganishe maeneo ya wafugaji na wakulima, ili kudhibiti migogoro inayopoteza maisha ya watu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumanne, tarehe 7 Septemba 2021, kwenye kikao cha wadau wa sekta ya mifugo, jijini Dar es Salaam.

“Mkulima anategemea mahindi na wewe mfugaji unategemea mifugo, kwa hiyo ni vizuri kila mmoja akaheshimu shughuli ya mwenzake.

“Serikali ya kijiji ipo igawe maeneo kubainisha wapi kunafaa kwa mifugo na wapi kunafaa kwa kilimo na tukaanzie hilo ili tuishi vizuri kwenye jamii yetu,” amesema Waziri Majaliwa.

Wakati huo huo, Waziri Majaliwa amewaomba wafugaji wasitumie watoto wadogo kuchunga mifugo, kwani hawataweza kuizuia mifugo hiyo isiingingie shambani na kuharibu mazao ya wakulima, hali inayochochea migogoro.

“Sitaki nikumbushie yaliyojitokeza karibuni Chalinze, raia mmoja ana shamba lake kapanda mahindi yake anakuja kuangalia mahindi anakuta ng’ombe wamejaa wanakula na mwenye ng’ombe hajali, tuache tabia ya watoto wadogo kuchunga,” amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema “ kwanza wanatakiwa waende shuleni, mbili hawana uwezo wa kukaa na kundi kubwa. Tuweke muelekeo mzuri wa ufugaji, tukabidhi vijana wenye uwezo wa kutafakari anajua hapa anapokwenda ng’ombe si penyewe halafu anamuepusha vinginevyo tutaleta madhara makubwa.”

Aidha, Waziri Majaliwa ameagiza lanchi zisizokuwa na mifugo mingi , maeneo yao yagawiwe kwa wafugaji ili kuwaepusha na adha ya kuhamisha mifugo kwa ajili ya kutafuta malisho.

“Serikali imeweka azma ya kutenga maeneo ya mifugo, tumeagiza lanchi ambazo hazina mifugo tukate maeneo tuwaweke wafugaji wenye mifugo mingi, walishe hapo,” amesema Waziri Majaliwa.

Pia, Waziri Majaliwa amewashauri wafugaji kuchimba visima au mabwawa ili wapate maji ya kuhudumia mifugo yao kwa ajili ya kukwepa kuipeleka katika vyanzo vya maji.

error: Content is protected !!