August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa apigia debe uwekezaji nchini

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Ltd kinachotengeneza vinywaji baridi pamoja na kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili (mabo) cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, vilivyoko katika eneo la Iyunga Mjini Mbeya, anaandika Mwandishi Wetu.

Amevitembelea viwanda hivyo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa sera ya kujenga uchumi wa viwanda nchini, ambao ndiyo kipaumbe cha Serikali ya Awamu ya Tano.

Majaliwa alivitembelea viwanda hivyo akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.
Akiwa katika kiwanda cha Pepsi, alikagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi na wa kiwanda hicho kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa vinywanji baridi kwenye chupa za plastiki.

Alishauri kampuni hiyo kuendelea kupanua uwekezaji wake hapa nchini kwa kuwa Tanzania ina sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.

Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1999 kikiwa na wafanyakazi 75 na kwa sasa kina wafanyakazi 190.

“Nawashauri muendelee kuwekeza Tanzania kwani mbali na utulivu wa kisiasa pia sera na mazingira yake ya uwekezaji ni mazuri.” amesema

error: Content is protected !!