Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa alitaka baraza la michezo AU kukuza michezo, “tusikubali kushika mkia”
Habari Mchanganyiko

Majaliwa alitaka baraza la michezo AU kukuza michezo, “tusikubali kushika mkia”

Spread the love

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne kuweka nguvu katika kuhakikisha wanakuza na kuendeleza michezo kwa Ukanda huo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea.)

Amesema hayo leo Alhamisi tarehe 4 Mei 2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV Jijini Arusha.

Amesema kuwa mawaziri hao wawekeze kwenye kujenga uwezo wa kitalaamu ili kuzalisha wanamichezo wanaoweza kuleta mageuzi kwenye Sekta ya Maendeleo ya Michezo na Maendeleo kupitia Michezo “Tusikubali kushika mkia kila siku na wala tusikubali kurudi nyuma”.

Amesema kuwa lengo la kila taifa ni kuona timu yake inashinda makombe ya Kimataifa hasa Kombe la Dunia. “Tukiamua kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo na ujuzi pamoja na kushirikiana tunaweza kufikia malengo makubwa kwenye sekta ya michezo”

“Tunapaswa kufika mahali pa kuona kuwa Tanzania ikishinda wote tumeshinda, Uganda ikishinda, wote tumeshinda, Ethiopia ikishinda wote tumeshinda. Tushirikiane ili tuwe mfano na kielekezo kwa Kanda nyingine za Mabaraza ya Michezo ya Umoja wa Afrika,” amesema.

Katika Hatua nyingine, Majaliwa amewataka wajumbe wa mkutano huo kuichagua Tanzania kuwa makao makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Ukanda wa IV katika uchaguzi utakaofanyia mapema leo Mei 04, 2023.

Amewaeleza wajumbe hao kuwa Tanzania ina kila sababu ya kupigiwa kura ya ndiyo kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuipa hadhi sekta ya michezo nchini.

Amesema kuwa uwepo wa mageuzi makubwa katika diplomasia ya michezo ya kimataifa ambapo chini ya uongozi thabiti wa Serikali timu za Taifa za Tanzania na vilabu zinafanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa “jambo hili linatia hamasa kwa wanachama kuona kuwa Tanzania inapiga hatua katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

“Uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kwenye Miundombinu ya Michezo ikiwemo ujenzi wa Viwanja Vikubwa na vizuri vya Michezo vinavyokidhi viwango vya Kimataifa vya CAF na FIFA. Mathalan, Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa ambao hutumiwa kwa Michezo ya Kitaifa na Kimataifa  ikiwemo Timu ya Taifa ya Brazili na Klabu ya Everton ambazo pia zimewahi kuutumia,” amesema.

Katika Mkutano huo, Rais Dk. Samia Aliwasilisha ujumbe maalumu kwa wajumbe na Mawaziri wa michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne kuichagua Tanzania kuwa makao makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Ukanda wa IV.

“Niwahakikishie kuwa Tanzania inauzoefu wa kuwa makao makuu ya taasisi mbalimbali za kimataifa, na pia Tanzania ina miundombinu yote muhimu ambayo itaiwezesha baraza hilo kufanya kazi kwa ufanisi,” amesema Rais Samia.

Naye Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Dk. Pindi Chana amesema kuwa tasnia ya michezo ni kati ya sekta ambazo inatoa ajira kwa vijana wengi “sekta ya michezo kwenye nchi wanachama ilitunga sheria ili kuendelea vipaji, michezo inaiunganisha Afrika kuwa moja”

Ameongeza kuwa wataendeleza mapitio ya sheria kanuni na taratibu ili kuendelea kuikuza sekta ya ya michezo kwa kuwa michezo ni biashara na chanzo cha uhakika cha ajira kwa vijana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!