Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa akoshwa ujenzi wa madarasa Lindi, mamilioni yabaki
Habari za Siasa

Majaliwa akoshwa ujenzi wa madarasa Lindi, mamilioni yabaki

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameridhishwa na hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa madarasa yanayotokana na fedha za maendeleo mkoani Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Ametoa kauli hiyo jana Jumanne, tarehe 28 Desemba 2021, wakati akizungumza na viongozi wa mkoa huo kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea mara baada ya kupokea taarifa ya kila wilaya.

“Nimefurahi kusikia kuna maeneo kazi imekamilika kwa asilimia 100, wilaya nyingine zimefikisha asilimia 97, nyingine asilimia 75, na kikubwa zaidi ni kuweza kubakiza fedha baada ya kazi kukamilika,” alisema Majaliwa

“Wilaya moja imebakiza Sh.35 milioni, nyingine Sh.33 milioni na nyingine zaidi ya Sh.10 milioni. Hii ni dalili njema kwamba kazi hii ilisimamiwa vizuri, nawapongeza viongozi wote wa mkoa na wilaya, pamoja na wananchi waliojitokeza kuchangia nguvu kazi yao.”

Waziri Mkuu alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kutafuta fedha hizo ambazo zimekuwa mkombozi mkubwa kwenye kutatua changamoto mbalimbali katika huduma za kijami.

“Kwa fedha hii ambayo Rais ametumia jitihada kubwa kuzitafuta, na tumezipata tena kwa masharti nafuu, ni lazima tuzitumie ipasavyo. Nimefurahi sana kusikia nyie mmetumia vizuri fedha zenu kujenga madarasa na zimebaki.”

Majaliwa alisema kutokana na mfano uliooneshwa na mkoa wa Lindi, anataraji kusikia mikoa mingine pia ikiwa imekamilisha kazi na fedha zimebakia hasa kwenye mikoa ambayo malighafi na vifaa ni rahisi ama haitoki mbali.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na viongozi wa Serikali na CCM wa mkoa na wilaya za mkoa huo, Mkuu wa Mkoa Lindi, Zainab Tellack alisema hatua za ujenzi uliobakia ni hatua za kumalizia kuweka madawati, nyingine kupakaa rangi na chache sana ni kuezeka.

Alisema licha ya kazi kubwa iliyofanyika, baadhi ya wilaya zimebakiza fedha lakini nyingi zimebakiza vifaa vya ujenzi kama nondo, saruji na rangi.

“Tunataka tuombe kibali maalum cha kutumia hizi fedha zilizobaki na vifaa vilivyobakia ili kuboresha miundombinu kwenye maeneo mengine,” alisema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga alisema alipokea Sh.2.26 bilioni ambapo kati ya hizo, Sh.1.1 bilioni zilikuwa ni za ujenzi wa madarasa 56 katika Manispaa ya Lindi na mengine 58 katika Halmashauri ya Mtama kwa thamani ya Sh.1.16 bilioni.

“Katika Manispaa ya Lindi, tulikuwa na madarasa 35 ya shule za sekondari na madarasa 21 ya shule shikizi. Yote yameshakamilika kwa maana ya kuwekewa gypsum, marumaru na madirisha ya aluminium. Tumebakiza sh. milioni 35,” alisema.

Alisema katika Halmashauri ya Mtama madarasa 27 kati ya 58 yamekamilika kabisa na 31 yaliyobakia yako kwenye hatua tofauti. Alisema hapa hawajafikia hatua ya kubaini kiasi cha fedha kitakachobakia hadi wamalize kabisa kazi ya ujenzi na kuweka madawati madarasani.

Wilaya nyingine iliyofikisha asilimia 100 ya ujenzi ni ya Nachingwea. Wilaya hiyo ilipokea Sh.1.1 bilioni kwa ajili ya madarasa 69 ambapo madarasa 57 ni ya sekondari na 12 ni ya shule shikizi. Wilaya hiyo imebakiwa jumla ya Sh.3.7 milioni.

Wilaya ya Liwale bado haijakamilisha sababu ya changamoto ya umbali lakini Mkuu wa wilaya hiyo aliahidi atakamilisha kabla ya tarehe 31 Desemba 2021 kama ilivyoelekezwa na Serikali.

Wilaya ya Kilwa ilipokea Sh.2.06 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 103 ambapo madarasa 28 yamekamilika kwa asilimia 100 na yaliyobakia yako kwenye asilimia 75 ya ujenzi wake.

Majaliwa yupo jimboni kwake Ruangwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

1 Comment

  • WHICH NAME ALWAYS PRODUCES NICE WOMEN FOR MARRIAGE AS REPARATION OF FIRST LADY!

    1. LISA
    2. MARGRATE
    3. MARRY
    4. CATHELINE
    5. QUADRIYAH
    6. ELIZABETH
    7. JOSEPHINE
    8. JANET
    9. SASHA
    10. PRISCA
    11. ADELA
    12. JOYCE
    13. NYAMWIZA
    14. MAYA
    15. ADELAH
    16. ZAWAD
    17. GIFT
    18. SALIMA
    19. HALIMA
    20 ESTER
    21. ANNA
    22. ANASTAZIA
    23. SARAH
    24.
    POWER OF WOMAN ON NAMES?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!