Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa akerwa shule za Kiislamu kuungua moto
Habari Mchanganyiko

Majaliwa akerwa shule za Kiislamu kuungua moto

Spread the love

TUME ya kuchunguza matukio ya majengo ya Shule za Msingi na Semondaei za Kislamu kuungua kwa moto jijini Dar es Salaam inakamilisha taarifa yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam.

Hayo amesema leo Ijumaa tarehe 31 Julai 2020 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akizungumza katika  Baraza la Eid El Adh’haa  lililofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.

Tume hiyo imeundwa na Aboubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na mkoa hiyo ikishirikisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini.

Shule ya Sekondari ya Mivumo Islamic Seminary na Kinondoni Muslim ni miongoni mwa shule zilizoungua hivi karibuni.

Majaliwa amesema, Serikali ilimuagiza Kunenge kuunda tume hiyo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Aboubakar Zubeir, Mufti Mkuu wa Tanzania kuhusu matukio hayo kutokea mfululizo pasina chanzo chake kujulikana.

“Mheshimiwa Mufti na Waislamu wenzangu, mmezungumzia suala la madhara makubwa yanayoendelea sasa ya majengo yetu ya shule za sekondari na msingi kuungua moto jambo hili Serikali tunalipokea.”

“Mufti ulikuja ofisini kwangu kueleza namna ulivyopata masikitiko na Waislamu wote kwa majengo kadhaa kuungua moto na ukaeleza  umejitahidi kutaka kujua chanzo lakini mpaka sasa hujajua chanzo,” amesema Majaliwa.

Waziri mkuu huyo amesema, tume hiyo iko katika hatua za mwisho za uchunguzi huo, na kwamba hivi karibuni itawasilisha ripoti yake serikalini.

“Tayari mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliunda tume na bahati nzuri iliwashirikisha nyie ili wapite maeneo yote yaliyoungua moto, wafanye mahojiano wapate maelezo ya kina tujue chanzo ni nini,” amesema

“Tume inaendelea, iko katika hatua za mwisho wanakamilisha ripoti baada ya hapo, Mufti Mkuu tutakujulisha,” amesema Majaliwa.

Pia, ametumia fursa hiyo kusema, yeyote atakayebainika kujihusisha na matukio hayo iwe mtu binafsi au kikundi cha watu, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Majliwa amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kwa kushirikiana na kamati zao za ulinzi na usalama, zinadhibiti matukio ya shule kuungua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!