May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa aipongeza Simba, amwagia sifa Barbara

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameipongeza klabu ya Simba kwa kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupata ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya AS Vita kutoka Congo DR. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …(endelea).

Simba jana ilianza kampeni yake kwenye mchezo wa kundi A, na kufanikiwa kuibuka na pointi tatu kwenye ardhi ya Congo kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka na ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na Chriss Mugalu dakika ya 60 kwa mkwaju wa penalti.

Katika hotuba yake ya kuhalisha mkutano wa pili, kikao c ha 10 cha Bunge jijini Dodoma, Majaliwa alisema kuwa anaipongeza klabu hiyo kuingia hatua hiyo na kushinda mchezo wake wa kwanza huku hakuwa nyuma kumpongeza mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez kwa kutangaza utalii kupitia jezi za timu hiyo.

Barbara Gonzalez, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba

“Nitumie nafasi hii kumpongeza Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, mwanadada Barbara Gonzalez kwa ubunifu na kushirikisha Wizara ya Maliasili na Utalii na hivyo kulipa heshima Taifa letu kwa kulitangaza kupitia jezi yao kwa maneno VISIT TANZANIA huu ni uzalendo wa hali ya juu ambo unapaswa kupongezwa na kuigwa,” alisema Majaliwa

Simba mabyo kwenye michuano hiyo imepangwa kundi A, sambamba na timu za AS Vita ya Congo DR, Al Ahly kutoka nchini Misri na El Merreikh ya Sudan.

Tayari Simba imeshajikusanyia pointi tatu kibindoni na kuongoza kundi hilo na mchezo unaofuata watakuwa nyumbani kuikaribisha klabu ya Al Ahly, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Februari 2021.

error: Content is protected !!