Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa afuta likizo za watendaji Krismas, mwaka mpya kisa… 
Habari za Siasa

Majaliwa afuta likizo za watendaji Krismas, mwaka mpya kisa… 

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) yote nchini humo wahakikishe watendaji wote wa Mikoa, Wilaya, Halmashauri wasiende likizo ya sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa mwaka huu. Anaripoti Brightnes Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Majaliwa amesema, watendaji wanapaswa kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati na wawe wamekamilisha ifikapo tarehe 28 Februari 2021.

“Suala hili nitalifuatilia mwenyewe ili kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa chaguo la kwanza na la pili wawe wameingia madarasani kufikia Machi Mosi mwaka 2021.”

“Ukamilishaji wa vyumba hivyo pamoja na madawati ufanyike kwa kutumia vyanzo vyenu vya ndani vya fedha,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana  Jumatatu tarehe 7 Desemba  2020 alipozungumza na Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi.

Kikao hicho ambacho Waziri Mkuu alikiongozo kwa njia ya televisheni akiwa ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma kilihusu upokeaji wa taarifa ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2021.

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Majaliwa ameiagiza Ofisi ya Rais-Tamisemi ihakikishe kazi hiyo inakamilika kwa wakati  na amewataka watendaji hao wahakikishe ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa na utengenezaji wa madawati unafanyika usiku na mchana.

Awali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi, Gerald Mweri alisema kati ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, wanafunzi 970 watapangwa kwenye shule maalumu, 1,059 shule za ufundi, 1,280 bweni kawaida, 803,326 watapangwa katika shule za sekondari za kutwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera alisema katika mkoa wake wanafunzi wote waliofaulu watapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2021 kwa sababu awali walikuwa na upungufu wa vyumba 42 vya madarasa, ambapo wamejenga shule mpya saba zenye vyumba 26 vya madarasa na wamekamilisha maboma 56 na hivyo kuwa na ziada ya vyumba 36 vya madarasa.

Kiongozi huyo alisema, mkoa umeweka mkakati wa kuwapeleka wanafunzi wote waliofeli katika vyuo vya maendeleo ya wananchi ili kuwawezesha kupata stadi za maisha zitakazowawezesha kujitegemea. “Mpango huu tunautekeleza kwa awamu ya pili sasa.”

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema mkoa wake ulikuwa na upungufu wa vyumba 400 vya madarasa, hadi sasa tayari wamekamilisha ujenzi wa vyumba 380 na kwamba watahakikisha hadi tarehe 30 Januari 2021 watakuwa wamekamilisha ujenzi wa vyumba vilivyosalia na wanafunzi wote watachaguliwa katika awamu ya kwanza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!