Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa aeleza Tanzania inavyoboresha usafiri wa majini
Habari za Siasa

Majaliwa aeleza Tanzania inavyoboresha usafiri wa majini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua upanuzi wa Bandari ya Mtwara
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema malengo ya Serikali ni kuimarisha usafiri kwenye maziwa yote na bahari ili kuwawezesha Watanzania wafanye biashara na mataifa ya nje. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

“Malengo yetu ni kuruhusu mataifa ya nje yafanye biashara na Tanzania na  kuruhusu Watanzania wasafiri kwenda hukohuko kuona na kujifunza ili warudi hapa na taaluma mpya.”

“Utaratibu huo pia utawezesha kutengeneza mzunguko mzuri wa kifedha kwa wananchi,” amesema Majaliwa.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu, imesema Majaliwa amesema hay oleo Jumanne tarehe 7 Julai 2020 wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya Klabu ya Bandari mjini Mtwara.

Waziri mkuu amesema  kabla ya kukagua ujenzi wa gati namba 2 katika bandari ya Mtwara juzi alitembelea miradi ya ujenzi wa bandari za Karema (Katavi), Kabwe na Kasanga (Rukwa) katika mwambao wa Ziwa Tanganyika.

“Nimetoka Ziwa Tanganyika ambako tunapakana na Burundi, Rwanda, Zambia na Congo na Serikali kwenye mkakati huu tumeingiza fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa bandari zetu. Tumeimarisha bandari ya Kigoma pale Kibirizi, kazi imekamilika na sasa tunajenga eneo la kuweka makontena,” amesema.

Mafunzi wakiendelea na ujenzi wa upanuzi wa Bandari ya Mtwara

Amesema katika Ziwa Victoria, kuna meli iliyokuwa inakarabatiwa na imeanza majaribio ya kwenda Kagera na nyingine inaendelea kujengwa ili kuruhusu wafanyabiashara wa Kanda ya Ziwa wafanye biashara zao kwa urahisi.

Katika hatua nyingine, waziri mkuu amewataka vijana wanaopata ajira kwenye miradi mikubwa inayogharimiwa na Serikali watumie fursa hiyo kupata utaalamu utakaowawezesha kuajiriwa maeneo mengine hata baada ya miradi ya sasa kukamilika

Akizungumza na vijana wa Kitanzania wanaofanya kazi kwenye mradi wa gati jipya katika bandari ya Mtwara leo mchana, Majaliwa amewataka vijana wote wanaofanya kazi kwenye miradi mbalimbali nchini hasa ile mikubwa na ya kimkakati wawe waaminifu ili kujenga taswira nzuri  ya nguvu kazi ya vijana wa Kitanzania wanapohitaji kuajiriwa hasa na makampuni ya nje ya nchi.

“Kuweni mabalozi wazuri wa vijana wenzenu kwa kufanya kazi kwa bidii na uaminifu wa hali ya juu ili mkimaliza miradi ya sasa, mpate ajira tena kwenye miradi mingine. Bado Serikali yetu inakusudia kuanzisha miradi mingine mingi  na matarajio ni kuwa vijana wa Kitanzania watanufaika kwa kupata ajira katika miradi hiyo.”

Awali, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Mhandisi Juma Kijavara alimweleza waziri mkuu kuwa kazi ya ujenzi wa gati namba 2 katika bandari ya Mtwara unafanywa na kampuni ya MS China Railway Construction Enginereering Group Company Limited (CRMBEG) kwa gharama ya Sh. 157.8 bilioni.

Amesema ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi tarehe 27 Mei, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Julai, 2020 ukisimamiwa na Mhandisi Mwelekezi, Inros Lackner kutoka Ujerumani.

Mhandisi Kijavara alisema, mradi huo umefikia  asilimia 75 ya utekelezaji wake na jumla ya Sh. 74.84 bilioni zimelipwa kwa mkandarasi sawa na asilimia 48.

Akizungumzia ushiriki wa wazawa katika ujenzi wa mradi huo, Mhandisi Kijava alisema mkandarasi huyo ameajiri wazawa 308 sawa na asilimia 87.5 ya wafanyakazi wote. Alisema wafanyakazi hao wameajiriwa katika  kada mbalimbali.

Katika ziara hiyo, waziri mkuu alifuatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kapteni mstaafu, George Mkuchika, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa na baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Mtwara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!