Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaliwa acharuka wasoma mita kubambika bili, “wanaichafua serikali”
Habari Mchanganyiko

Majaliwa acharuka wasoma mita kubambika bili, “wanaichafua serikali”

Spread the love

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya wasoma mita za maji nchini kuacha tabia ya kuwabambikia wananchi bili kubwa za maji kwani hatua hiyo inaichafua serikali jambo ambalo halitovumilika.

Pia ametoa muda wa siku 14 kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuwaunganishia maji wananchi wanaozunguka tenki kubwa la maji lililopo maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wanne kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Ndugu Kiula Kingu (mwenye kipaza sauti) juu ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji kutoka Makongo hadi Bagamoyo unaotarajiwa kunufaisha wakazi 450,000

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Machi 2023 wakati akizindua wiki ya maji iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa usambazaji wa maji kati ya Makongo na mji wa Bagamoyo.

Amesema kumekuwapo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa maeneo ya Hedari na Same kwamba wanabambikiwa bili kubwa za maji kama vile wana viwanda katika nyumba zao.

Amesema ubambikaji huo wa bili umekuwa ukiichafua serikali jambo ambalo kamwe viongozi wa Serikali na mamlaka husika hazitokubali.

“Nisisitize hakuna mtu anatozwa bili kubwa kama anakiwanda, viwango vya malipo vinafahamika, ni vizuri ni kuchangia huduma ila kama una kiwanda hicho ni kitu kingine,” amesema.

Ameitaka DAWASA kukamilisha michakato ya kununua mita za kisasa ili kila mwananchi alipie bili kulingana na maji anayotumia na kiwango cha bili ambacho anakiona.

“Hivyo wasoma mita wasitumie nafasi hiyo kuchafua serikali kwa kulazimisha bili, tukikugundua tutashughulika na wewe hapohapo,”amesema.

Pia ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa iwapo mamlaka zinazowaunganishia maji zinataka rushwa.

Amesema kwa kuwa gharama za kuunganisha maji kwa mara ya kwanza zinafahamika, wananchi nao watambue haki yao na pindi kutakapotokea urasimu katika uunganishiwaji wa maji watoe taarifa kwa mamlaka husika.

“Usikubali mtu yeyote awe mtumishi wa Dawasa au kiongozi, akuombe rushwa ya kuunganisha maji, hakuna rushwa utakayotoa maji kuja kwako, uunganisha ni wa gharama zilezile,” amesema.

Aidha, amesema mradi huo wa tenki la maji Tegeta jijini Dar es Salaam unatarajiwa kunufaisha wananchi 450,000 kutoka maeneo ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam hadi Bagamoyo mjini.

Pia ametoa wito kwa wananchi na wakurugenzi wa mabonde kuvilinda vyanzo vya maji ili kusitokee ukame kama uliotokea mwaka jana.

Awali Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alitoa wito kwa wananchi kuvunja ukimya na kutoa taarifa kwa viongozi na mamlaka zinazohusika pindi wanapobambikiwa bili za maji na wasoma mita.

“Hatutokubali kumuona msoma mita akimbambikizia mwananchi bili ya maji, niwaombe wananchi Rais Samia Suluhu Hassan ametuamini sisi viongozi wenu hivyo sehemu ambayo unapata changamoto usikae kimya, sisi viongozi tupo, atakayekuzinga tutashughulika naye hata awe na mapembe kiasi gani,” amesema Aweso.

Aidha, amesema katika bajeti zilizopita, fedha za maji zilizotolewa kwa asilimia 50 hadi 60 lakini katika uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, fedha za wizara hiyo katika miradi ya maji zimetolewa kwa asilimia 90.

1 Comment

  • A. UTANGULIZI
    1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2022/23 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba kwa Mwaka 2023/24. (Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanaume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani – VITA IMEZIDI)

    2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwasilisha Hotuba hii muhimu mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya kipekee kabisa namshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini kuendelea kusimamia Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ili kufikia matarajio ya Watanzania katika Sekta ya Ujenzi wa Nyumba Unaoisha na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa.

    3. Mheshimiwa Spika, vilevile kwa dhati nampongeza Mhe. Rais kwa namna anavyoiongoza Serikali ya Awamu ya Sita inayosimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, ambapo mafanikio mengi yamepatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ambapo WATANZANIA WOTE WANALALA KWENYE NYUMBA ZAO IFIKAPO USIKU WA SAA 1 BILA KUZINGATIA INAMILIKIWA YEYE MWENYEWE AU KUPANGA. Mafanikio hayo yameendelea kuitangaza nchi yetu siyo tu katika Bara la Afrika bali Duniani kote.

    4. Mheshimiwa Spika, ninaomba nitoe Rai kwa wananchi na Waheshimiwa Wabunge wote bila kujali itikadi za aina yoyote, tuendelee kuyaenzi mafanikio haya makubwa na kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

    5. Mheshimiwa Spika, vilevile, nitumie fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Viongozi Wakuu wa Kitaifa, ambao ni Makamu wa Rais, Dr. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr Hussein Ali Mwinyi kwa hekima kubwa katika kumsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza nchi yetu.

    6. Mheshimiwa Spika, pia, nimshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwani amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM na maelekezo mbalimbali ya Mhe. Rais pamoja na kusimamia vema shughuli za Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ndani na nje ya Bunge, AMBAO INAKUSUDI HADI KUFIKIA 2024 KILA MTANZANIA HATAKIWA KUJENGA TENA KWA MUJIBU WA SHERIA NA KUWAACHIA NHC NA TBA KUJENGA NYUMBA ZILIZO NA VIWANGO VYA KIMATAIFA.

    7. Mheshimiwa Spika, ninakushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba na YAO Mhe. TAN L. VIAZI (Mb.) na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kamati hii imefanya kazi nzuri na kutoa ushauri wa kuboresha mambo mbalimbali ikiwemo kupitia na kuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba na Taasisi zake kwa mwaka 2022/23.

    Ripoti ya Dunia ya Dawa za Kulevya ya UNODC 2022 inaangazia UPATIKANAJI WA DAWA ZA KULEVYA AMBAPO ASILIMIA 34 – 67 YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA COCAINE YAMEKUTWA KWENYE MADAPO YA KUTUPIA TAKA KATIKA MIJI YA IRINGA, MOROGORO, DODOMA NA DAR ES SALAAM… AIDHA, Mwelekeo wa kuhalalisha bangi baada ya kuhalalishwa, athari za kimazingira za dawa haramu, na matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanawake na vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!