August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa aagiza utoaji anwani za makazi kuwa endelevu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza Wizara zote, Sekretarieti za mikoa na Serikali za mitaa kuhakikisha zoezi la utoaji anwani za makazi linakuwa endelevu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Majaliwa amesema zoezi hilo limefikia asilimia 95 hadi sasa ambapo taarifa za anwani za makazi zaidi 12 zimeshatolewa.

Waziri Mkuu ametoa maelekezo hay oleo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa hotuba ya kuhitimisha Mkutano wa saba wa bunge la 12.

“Wizara zote, Sekretarieti za mikoa na Serikali za mitaa endeleeni kushughulikia changamoto zote zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa operesheni za anwani za makazi na kuhakikisha kwamba zoezi hilo linakuwa endelevu.”

Mbali na hayo pia Majaliwa ameagiza taasisi zote zenye dhamana ya ardhi na makazi kuhakikisha zinakuja na mikakati dhabiti ya kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi iliyoanishwa wakati wa operesheni ya anwani za makazi.

Aidha ameziagiza kutoa miongozo ya namna bora ya kushughulikia changamoto za watanzania wanaoishi katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria “ili kuhakikisha wananchi hao wananufaika na fursa za kuwa na anwani za makazi.”

Vilevile ameiagiza Wizara ya Habari na Teknolojia ya Habari kuhakikisha kuwa mpango wa uendelezaji wa mfumo unaotoa mwongozo wa shughuli zote za anwani za makazi utakavyofanyika kuhakikisha zoezi hilo kuwa na thamani wakati wote.

Viongozi katika ngazi zote hususan katika Tawala za mikoa na Serikali za mitaa wametakiwa kuhakikisha jamii inaendelea kuelimishwa ili kujua manufaa sanjari na kulinda miundombinu ya anwani za makazi kwenye maeneo yao.

Aidha ameagiza uhakiki wa majina ya mitaa katika vibao uendele kuanyika ili kujiridhisha usahihi wake na uonekano kwa mbali.

error: Content is protected !!