Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Majaliwa aagiza Uhamiaji kuzuia Paspoti za wakandarasi MV Mwanza
Habari MchanganyikoTangulizi

Majaliwa aagiza Uhamiaji kuzuia Paspoti za wakandarasi MV Mwanza

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Meli mpya ya Mv.Mwanza Hapa Kazi tu katika Bandari ya Mwanza Kusini.
Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza kuzishikilia paspoti za wafanyakazi wa Kampuni ya Gas Entec Ship-building Engineering ya nchini Korea ambayo inayojenga Meli mpya ya Mv. Mwanza Hapa Kazi tu katika Bandari ya Mwanza Kusinikwa kukiuka madharti ya mkataba wa kazi hiyo.

Ujenzi wa meli hiyo mpya inagharimu zaidi ya Sh billioni 97 ambapo mpaka sasa Serikali imelipa zaidi ya asilimia 80 ya fedha zote ilihali ujenzi wake umefikia asilimia 65 pekee. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkandarasi wa mradi huu amefukuza wafanyakazi zaidi ya 100 na kubaki na wafanyakazi 20 tu

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo tarehe 7 Mei, 2022 katika ziara yake ya siku nne ambayo ameanza kuifanya leo mkoani humo.

Amesema lengo la kuchukua uamuzi unatokana na Kampuni hiyo kuondoa wafanyakazi zaidi ya 100 waliokuwa wanajenga Meli hiyo na kubakiza wafanyakazi 20.

Amesema kwa mujibu wa mkataba ujenzi wa meli hiyo hadi kufikia leo Mei 7, 2022 ulitakiwa uwe umefikia asilimia 95.

Pia kampuni hiyo imeuza hisa kwa Kampuni nyingine bila Serikali kujua jambo ambalo ni kinyume na mkataba wa Kampuni hiyo na Serikali ya Tanzania.

“Nawaagiza Uhamiaji ichukue Passpoti zote za wakandarasi hadi meli ikamilike, nimezungumza na Balozi wa Korea ameridhia, nimewasiliana na Rais naye ameridhia,” amesema Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

error: Content is protected !!