July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaji waahidi uamuzi leo

Spread the love

MABISHANO ya kisheria yaligubika shauri linalohusu mpigakura kukaa au kutokaa umbali wa mitaa 200 kutoka eneo la kupigakura lililofunguliwa katika Mahakama Kuu na wakili anayetetea upande wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Peter Kibatala, kuitaka mahakama ieleze hatima ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Wakili Kibatala alidai haki imekiukwa baada ya Rais Jakaya Kikwete, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na IGP Ernest Mangu kwa nyakati tofauti kutoa alichokidai ni katazo kwa wananchi kuwa hawatakiwi kukaa katika maeneo ya kupigiakura na badala yake kurudi majumbani mwao.

Katika hoja zake, Kibatala anadai kuwa maoni yao wameona kuwa kifungu cha 104(1) kinampa ruhusa mwananchi kukaa umbali wa mita 200 au ndani ya umbali huo ili kushuhudia kinachoendelea na kuitaka mahakama itoe maana kamili wa kifungu hicho ili kuondoa utata.

Kwa upande wa Majaji wamedai kuwa katika kiambatanishi kinaeleza wanahitaji kukaa ndani ya mita 200 au umbali huo kutoka katika kituo cha kupigia kura ili kulinda kura zao ambacho pia majaji hao watatu, jaji Lugano Mwandambo, Sekiene Kihiyo na jaji Aloycious Mujulizi wamedai kuwa wananchi hawawezi kulinda kura badala yake mawakala ndio wanapaswa kufanya zoezi hilo “hakuna kipengele cha kulinda kura kwenye sheria.” Amesema jaji Mwandambo.

Upande wake wakili wa serikali Dk. Tulia Ackson alidai aonavyo, Kifungu cha 104(1), Sura ya 343 anakitafsiri kwa maada tatu ambapo (i) kinakataza kabisa mikutano ya kampeni siku ya uchaguzi (ii) kinataka mtu yeyote kutoonyesha alama au picha au sare ya kuonyesha chama fulani (iii) kukataza mtu yeyote kufanya shughuli ya kisiasa ndani ya mita 200 lakini mita hizo hazihusiani na mengine.

Ackson anadai wanaohitajika kufika baada ya kupigakura ni mawakala wa wagombea, wagombea wenyewe na wasaidizi wa uchaguzi pia Kifungu cha 72(1) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinasema “kama mtu hakutajwa katika 72(1) basi asiwepo.”

Kabla ya kumaliza hoja zote za mawakili wa Serikali na Chadema shauri lilisimama kwa muda wa dakika 10 kisha kusikilizwa tena hoja na hatimaye likaahirishwa hadi leo (22/10/2015) kwa maelekezo muhimu ya Mahakama kuamua hatima shauri hiyo.

Hata hivyo, walipofika mahakamani leo, majaji walisema wangali wanapitia kufanya uchambuzi wa vipengele vya sheria na kuahirisha kutoa uamuzi hadi kesho asubuhi.

error: Content is protected !!