Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Majaji Kenya wakimbia mahakama ya juu
Kimataifa

Majaji Kenya wakimbia mahakama ya juu

Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga
Spread the love

HAKAMA ya Juu Nchini  Kenya imeshindwa kusikiliza na kutoa maamuzi katika kesi ya kupinga kufanyika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika kesho kutokana na baadhi ya Majaji kushindwa kufika mahakamani.

Jaji  Mkuu,  David Maraga amesema baadhi ya majaji wapo nje ya nchi na kwamba wasingeweza kufika mahakamani kwa sababu mbalimbali.

Kesi  hiyo iliwasilishwa na wapiga kura watatu ambao walisema Tume ya Uchaguzi na Mipika ya Kenya (IEBC) isingeweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki kesho.

Miongoni  mwa Majaji waliokosa mahakamani ni pamoja na  Naibu Jaji Mkuu,  Philomena Mwilu ambaye hakuweza kufika mahakamani kutokana na dereva wake kupigwa risasi jana.

Jaji Ibrahim, ambaye amekuwa akiugua, yuko nje ya nchi. Majaji,  Smokin Wanjala na Jacktone Ojwang hawakuweza kufika kortini pia.

Jaji Njoki Ndung’u amesafiri nje ya jiji la Nairobi na hakuweza kupata usafiri wa kumuwezesha kufika mahakamani kwa wakati.

“Sisi wawili hatuwezi kufikisha idadi inayohitajika ya majaji mahakamani kwa mujibu wa kifungu 162 (2) cha Katiba.
Kesi imeahirishwa hadi wakati mwingine,” ametangaza Jaji Maraga.
Wakati hayo yakitokea mahakamani wafuasi wa upinzani wameendelea kuandamana katika ngome ya Bw Odinga mjini Kisumu.

Wakili wa raia hao watatu waliokuwa wamewasilisha kesi hiyo, Harun Ndubi, ameshutumu hatua ya majaji kukosa kufika mahakamani huku akisema ni jambo la kushangaza.

“Wanatoweka wakati tunawahitaji kutekeleza jukumu hili muhimu, unashangaa iwapo wanafuata kiapo walichokula,” amesema.

Katika ofisi za  IEBC mjini Kisumu ulinzi umeimarishwa kila kona ili kuhakikisha hakuna uharibifu wowote unafanyika.
Seneta wa Siaya James Orengo aliyewakilisha Raila Odinga mahakamani wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti amesema kilichotokea leo ni “mapinduzi ya katiba”.

“Haya yamekuwa yakifanyika, hata katika tume ya uchaguzi. Stakadhabi zilizowasilishwa na tume kujibu kesi zimewasilishwa na naibu mwenyekiti na wala si mwenyekiti.

”Ni wazi kwamba tume ya uchaguzi inafanya kazi bila mchango wa mwenyekiti na  Wafula Chebukati amekuwa abiria,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

KimataifaTangulizi

Boti yazama DRC, 80 wafariki dunia

Spread the loveJUMLA ya watu 80 wameripotiwa kufariki dunia huko nchini Congo...

error: Content is protected !!