MBUNGE wa jimbo la Uyui nchini Tanzania, Almasi Maige, amehoji sababu ya Tanzania kushindwa kupata nishati ya mafuta licha ya kuwa na viashiria vya mafuta vinavyyofanana na nchi zilizopata mafuta. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Maige amesema jambo hilo limfanya kujiuliza maswali kwamba huenda ni matumizi ya teknolojia duni, hujuma, utaalamu mdogo na kutokuwepo utashi.
Mbunge huyo amehoji hayo leo Alhamisi tarehe 2 Juni, 2022 bungeni jijini Dodoma akichangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati.
“Mimi sijui kwanini Tanzania hatujapata mafuta kwasababu wenzetu walikopata mafuta ni ushoroba uleule wa bonde la ufa na hapa kwetu limeanzia hapa. Najiuliza ni teknolojia ndogo ya utafutaji mafuta, utaalamu mdogo, hakuna utashi, hujuma, uwekezaji mdogo na mengine.”
Amemtaka Waziri Januari Makamba kulifanyia kazi “Makamba mimi nitakushika wewe kwasababu haya ni mambo yako kahakikishe tunapata mafuta.”
Amesema huko Wembeni Tabora kuna eneo limeonekana lina uwezekana wa kuwa na mafuta lakini uchunguzi ni mdogo unaofanyika “na wataalamu wanaokwenda hawabebi vifaa vikubwa.”
Pia alihoji sababu ya kukifanya kipaumbele cha utafutaji gesi na mafuta kuwa namba 11, “kwanini kisiiwe kipaumbele cha kwanza, hamtaki kupata mafuta?” alihoji.
Katika hotuba yake ya bajeti aliyoiwasilisha bungeni jana tarehe 1 Juni, 2022, Makamba amesema jumla ya vitalu vya kimkakati 11 vilifanyiwa kazi za utafiti wa mafuta na gesi katika mwaka wa fedha 2021/22 na tafiti hizo zipo katika hatua mbalimbali.
Leave a comment