April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahujaji wa DRC wazuiwa kuingia Makka kisa Ebola

Spread the love

NCHI ya Saudi Arabia imegoma kutoa hati ya kusafiria ‘Viza’ kwa mahujaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikihofia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza kwamba nchi ya DRC ina mlipuko wa Ebola.

Wizara hiyo imesema hatua hiyo ya kuzuia watu kutoka DRC kuhiji Makka ni kulinda usalama wa mahujaji kutoka katika mataifa mengine.

Imamu Djuma Twaha, Kiongozi wa Waislamu nchini DRC amesema watu 410 nchini humo walipanga kwenda kuhiji mjini Makka mwezi huu.

error: Content is protected !!