Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maharage, mahindi yaongeza mapato Kasulu
Habari Mchanganyiko

Maharage, mahindi yaongeza mapato Kasulu

Spread the love

ELIMU ya kilimo bora cha mazao ya mahindi na maharagwe, inayotolewa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kupitia Mradi wa Kigoma Pamoja Program (KJP), imefanikiwa kuongeza mapato kwa Halmashauri ya Kasulu Mji mkoani Kigoma hadi kufikia Sh. milioni 200. Anaripoti Selemani Msuya, Kasulu… (endelea).

Mradi KJP unatekelezwa katika wilaya za Kasulu,. Kibondo na Kakonko, unashirikisha mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) 16, eneo la kilimo unatekelezwa na WFP, Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC), Shirika la Uendelezaji wa Mitaji la Umoja wa Mataifa (UNCDF) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).

Mkulima wa mahindi katika Kijiji cha Nyumbigwa, Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma, Mirambo Masudi akiwa akiwaeleza waandishi nama WFP walivyombadilisha katika kilimo chake, huku akiwa ameshika kapu kwa ajili ya kuvuna mahindi kwa njia bora na salama.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa KJP Wilaya ya Kasulu, Masalu Charahani wakati  akizungumza na mwandishi wa habari hii ambaye alikuwa katika ziara ya kuangalia namna mradi huo ulichangia mafanikio kwa wakulima na halmashauri.

Charahani alisema kabla ya mradi huo kufika Halmashauri ya Mji Kasulu kilimo cha maharagwe na mahindi kilikuwa kinachangia mapato kidogo ila kwa miaka miwili ya mradi mapato yameongezeka kwa kiwango kikubwa.

Mkulima Zipora Mussa wa kijiji cha Nyumbigwa Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma akieleza waandishi wa habari namna WFP kupitia KJP ilivyochangia kuongeza uzalishaji wa mahindi.

“Kabla ya mradi ushuru wa zao la maharagwe ulikuwa hauzidi Sh.milioni 150 ila kupita elimu na mafunzo waliyopata wakulima tunakusanya ushuru hadi Sh.milioni 200. Hivyo hivyo kwenye mahindi tulikuwa tunakusanya Sh.milioni 50 ila sasa tunakusanya zaidi ya Sh.milioni 100,” alisema.

Alisema WFP, FAO, UNCDF na ITC wamehusika kwa asilimia kubwa kwa Halmashauri Mji Kasulu kuongeza mapato, hivyo watahakikisha hawayaangushi mashirika hayo ya kimataifa.

Charahani alisema WFP imekuwa ikitoa elimu kuhusu namna ya kuvuna, kuhifadhi na kuwapatia wakulima vifaa kama maturubai, mashine ya kupima unyevu, mashine za kupukuchua mahindi na mengine mengi.

Mratibu huyo alisema WFP kwa kushirikiana na Serikali wametoa mafunzo ya namna ya kuandaa shamba, kuvuna na kuhifadhi mazao kwa wakulima 3,000.

“Tumepokea mashine tatu ya kupukuchua mahindi, ambapo mashine hizo zinaweza kupukuchua magunia 25 kwa saa mbili na kutumia lita moja, hivyo ukiwa na lita mbili unapukuchukua gunia 50 za mahindi,” alisema.

Mratibu huyo alisema WFP wamefanikisha Mji wa Kasulu kuwa na vyama vitatu vya ushirikia ambavyo ni Kaluta, Mwamwe na Mulambia na kwamba halmashauri ipo katika mpango wa kujenga maghala mapya kwenye kata ambazo hazina.

Akizungumza kuhusu mradi huo Mzee Sospeter Mkula wa Kijiji cha Nyumbigwa alisema WFP wamemuwezesha kulima kilimo cha kisasa ambapo anatumia eneo dogo anapata mavuno mengi.

“Nawashukuru WFP na wadau wengine ambao wametujengea uwezo wa namna ya kuandaa shamba, kuvunia, na kuhifadhi. Elimu hii imesadia kupata mazao bora ambayo thamani yake inakuwa juu,” alisema.

Kwa upande wake Mirambo Masudi alisema mradi huo wa KJP ambao unatekelezwa na WFP umemuongezea hamasa ya kutaka kulima kwani ana uhakika wa kupata chakula cha familia yake na soko ndani na nje ya nchi.

Kaimu Mkuu WFP Kasulu Mkoa wa Kigoma, Michael Bisama akielezea namna shirika hili lilivyoinua wakulima wilayani hapo kupitia Mradi wa KJP.

“Sisi tulikuwa tukivuna tunayatupa chini, matokeo yake mahindi yanakuwa machafu na hayana ubora unaohitajika, hivyo tunakula chakula kichafu, lakini baya zaidi hata kama unataka kuuza unauza kwa bei ndogo,” alisema.

Mkulima Zipora Mussa alisema mafunzo ambayo wamepata kupitia WFP kwenye na mradi KJP yametoa matokeo chanya kwake na wakulima wenzake ambao walikuwa wanaandaa mashamba na kuvuna kizamani.

Zipora alisema pia WFP imewapatia mashine ya kupukuchua mahindi wa muda mfupi jambo ambalo linawawezesha kufanya kazi zingine za uzalishaji, hivyo kuongeza kipato.

“Mimi nalima heka moja na nusu ya mahindi ambapo hali ya hewa ikiwa nzuri napata hadi gunia 15, jambo ambalo awali ilikuwa ngumu. Ila mahindi yangu nikipeleka sokoni kwa sababu ni bora nauza kwa haraka,” alisema.

Mkuu wa Programu za WFP wilayani Kasulu, Michael Bisama alisema uwekezaji waliwekeza umetoa matokeo chanya hivyo kuiomba Serikali kuendeleza mpango huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!