October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maharagande ajitosa rasmi ubunge Segerea

Spread the love

MBARALA Maharagande, Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu Taifa wa Chama cha ACT-Wazalendo, amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Segerea jijini Dar es Salaam, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Maharagande amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumatano tarehe 1 Julai 2020 na Athuman Maarufu, Katibu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Jimbo Segerea.

Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Maharagande amesema, ameanza rasmi safari ya kuliwania jimbo hilo lililokuwa mikononi mwa Chama cha Mapinduzi (CCM), chini ya Bonah Kamoli.

“Safari imeanza rasmi, leo nimechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Segerea katika mchakato ndani ya chama,” amesema Maharagande.

 Chama cha ACT-Wazalendo kimefungua rasmi pazia la uchukuaji na urejeshaji fomu za kugombea urais ubunge, uwakilishi na udiwani leo, ambapo linatarajia kukoma tarehe 13 Julai mwaka huu.

error: Content is protected !!