August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama zabanwa mbavu

Spread the love

MAHAKAMA nchini zimetakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia haki ili kurudisha imani kwa wananchi, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Fredinand Wambali, Jaji Mkuu Kiongozi wa Mahakama Kuu wakati akifungua mkutano wa siku 10 wa mpango kazi uliowahusisha watendaji wa mahakama wa mikoa, manaibu, wasajili na uongozi wa Mahakama Kuu.

Amesema, watumishi wa ngazi zote katika mahakama wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia haki bila kuwepo uonevu wa aina yoyote.

“Wananchi wengi wanalalamikia mienendo ya maofisa wa mahakama, lakini mkae mkijua kwa mazingira yoyote yale mtumishi au ofisa hatakiwi kulalamikiwa akiwa katika sehemu yake ya kazi au nje ya kazi.

“Unaweza kuona ni jinsi gani ambavyo labda karani wa mahakama anafanya vitu vya ovyo, jambo hilo linaweza kusababisha kuonesha mwonekano mbaya katika kazi,” amesema Jaji Kiongozi Wambali.

Amesema “kuonesha kuwa wananchi wanakuwa na imani na mahakama, ni wazi pale mtakapoona kuwa rufaa zimepungua kukatwa.”

Mbali na hilo Jaji Wambali amesema, ili kuondokana na migongano mahakama inataka kuishauri tume kuanzishwa kwa kanuni za watendaji.

Na kuwa, hatua hiyo itasaidia kuwepo kwa utendaji wenye ufanisi mkubwa katika na kufanya jamii kuwa na imani na mahakama.

Katarina Revokati, Msajili wa Mahakama nchini amesema, umefika wakati sasa wananchi kuwa na imani kubwa na mahakama.

Na kuwa, ni wakati wa kuwafikia wananchi katika maeneo ambayo hayafikiki badala ya kusubiri wananchi waifuate mahakama.

Mbali na hilo amesema, kwa sasa malalamiko yameanza kupungua jambo ambalo linaonekana kujenga imani kati ya wananchi na mahakama.

Amesema, katika kufanya kazi ni vyema hakimu akafanya kazi yake na mtu akichukulia kuwa, siyo mtu mwenye hatia hadi hapo itapabainika kuwa mtu hugo ana hatia.

“Wakati mnapokuwa mkisikiliza mashauri, chukulia kuwa mtu huyo hana hatia na anapojitetea mchukulie anajitetea kwa nia njema.

“Itakabobainika kuwa mtu huyo ana hatia, basi haki itendeke kwa bila kuwepo na malalamiko,” amesema Revokati.

 

error: Content is protected !!