Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yaweka zuio kina Mdee kutoswa bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yaweka zuio kina Mdee kutoswa bungeni

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio la muda la kutofanyika chocholate kwenye ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka maombi yao ya msingi yatakaposikilizwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …. (endelea).

Mdee na wenzake wameamua kurudi tena mahakamani baada shauri lao namba 16 la mwaka 2022 kutupiliwa mbali na Jaji John Mgetta tarehe 22 Juni 2022.

Jaji Mgeta alitupilia mbali shauri hilo kwa kile alichosema ni mapungufu ya kisheria yaliyomo kwenye maombi hayo ikiwa pamoja na kukosea kuandika Board Of Trustee badala ya The Registed Trustee Board na kuwasilisha mashtaka yao kwa kukosea.

Leo Jumatatu, tarehe 27 Juni 2022 mbele ya Jaji Mustapha Ismail mawakili wanaowawakilisha kina Mdee waliiomba Mahakama hiyo kutoa amri ya zuio huku wakingoja kusikilizwa kwa maombi hayo.

Wakati huo huo wajibu maombi namba moja (Chadema) waliwasilisha mapingamizi matatu mahakamani hapo.

Esther Matiko

Upande huo uliwakilishwa na Peter Kibatala umeweka mapingamizi matatu yaliyoegemea kwenye hati ya kiapo ya waombaji.

Kwa mujibu wa Mahakama hiyo Ubunge wa kina Mdee utaendelea mpaka tarehe 29 Juni 2022 Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi hayo.

Mbali na Mdee, wengine waliofukuzwa Chadema, ni waliokuwa wajumbe wa Kamati
Kuu (CC), Esther Matiko na Ester Bulaya; aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara), Hawa Subira Mwaifunga na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Wengine, ni aliyekuwa Katibu mkuu wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), Nusrat Hanje; aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Bawacha (Bara), Jesca David Kishoa; Cecilia Pareso, Agnesta Lambart, ambaye alikuwa mwenezi wa Bawacha na Tunza Malapa, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, mkoani Mtwara.

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

Katika orodha hiyo, wamo pia Asia Mohammed, aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Bawacha (Zanzibar), Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Flao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

Mdee na wenzake walifungua maombi mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jambo ambalo lilikuwa linawafanya kupoteza sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Walifikia uamuzi wa kukimbilia mahakamani, baada ya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, kuamua tarehe 27 Novemba 2020, kuwavua uanachama na baadaye mkutano wa Baraza Kuu wa 11 Mei 2022, kusikiliza rufaa zao na kufikia uamuzi wa kuwatimua.

Chadema walifikia uamuzi wa kumtimua Mdee na wenzake, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA), kufuatia kupatikana na makosa ya usaliti, kughushi nyaraka za chama na kisha kujipeleka bungeni kujiapisha kuwa wabunge, kinyume na maelekezo ya chama chenyewe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!