April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yaweka kiporo kesi ya Meya Dar

Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Spread the love
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kutolea maamuzi maombi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, kuzuia baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo, kumuondoa katika kiti chake. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Isaya amewasilia ombi hilo, akiomba mahakama hiyo, kutoa zuio la kuitishwa kwa kikao cha kumjadili na baadaye kumuondoa  madarakani.

Maombi ya meya huyo yamewasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Hekima Mwasipu.

Katika hati yake ya kiapo, wakili Mwasipu ameimba mahakama kumuelekeza mkurugenzi wa jiji, mwanasheria wa jiji, mkuu wa mkoa na au mtu mwinge yeyote kuitisha kikao chenye ajenda ta kumjadili na meya huyo na kumuondoa kwenye nafasi yake, mpaka hapo kesi yake ya msingi itakaposikilizwa.

Mwasipu amesisitiza kuwa ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano, inaelekeza kuwa wakati haki ya mtu inaposikilizwa na mhakama au chombo chochote, ana haki ya kupewa nafasi ya kusilikizwa.

Akjibu hoja hizo, Gabriel Malata, wakili kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa  Serikali, ameeleza kuwa maombi hayo yameletwa chini ya hati ya dharula na wito waliopelekewa uliwaita kuja kusikiliza kesi na sio kusikiliza maombi ya zuio.

Amesema “hoja ya zuio la kumuondoa kwenye umeya ni kitu ambacho hakijulikani, na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa tuhuma za mitaani.

“… na kwamba, hakuna mazingira yoyote yaliyokuwa wazi isipokua kuna hisia, na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa kitu ambacho hakipo kwenye maombi.”

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi kesho Alhamisi tarehe 9 Januari 2020 saa 8 mchana, ambako Hakimu Mkazi Janeth Mtega, anatarajia kutoa uamuzi.

Isaya ambaye alipatikana baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa 25 Oktoba 2015, ametuhumiwa na madiwani wa CCM kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya jiji la Dar es Salaam, Isaya anadaiwa kutotumia kiasi cha Sh. 5.8 bilioni, zilizotokana na mauzo ya hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ambalo lilikuwa mali ya jiji.

Shirika la UDA, ambalo mwaka 1983 Msajili wa Hazina alitoa asilimia 51 ya hisa kwa Halmashauri ya Jiji, huku serikali kuu ikibakiwa na asilimia 49, liliuzwa kinyemela na Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.

error: Content is protected !!